Na Bertha Lumala,Tanga
Kikosi cha mabingwa mara 24 waTanzania Bara, Yanga SC kimefanya kweli jijini hapa baada ya kuichapa Coastal Union bao 1-0 katika mechi pekee ya leo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ushindi huo umeifanya Yanga SCiwang’oekileleni Azam FC ikifikisha pointi 22,moja nyuma ya wanalambalamba ambao hata hivyo, wana mechi moja mkokoni.
Katika mechi hiyo ya kiporo ya raundi ya 10 iliyopaswa kuchezwa jijini hapa Januari 10 lakini ikapigwa kalenda na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na ushiriki wa Yanga SC katika Kombe la Mapinduzi, watoto wa Jangwani walicheza kwa kujihamia zaidi wakishambulia kwakushtukiza.
Bao pekee la mechi limefungwa na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kurushwa kama kona wa Mbuyu Twite dakika ya 12 ya mchezo.
Coastal Union wanaonolewana Mkenya James Nandwa walijaribu kulishambulia kwa kasi muda wote lango la Yanga SC baada ya kufungwa kwa bao hilo lakini hawakufanikiwa kupata bao kutokana na umahiri wakipa Ally Mustafa ‘Barthez’ ambaye muda mwingi alikuwa akijiangusha kupoteza muda baada ya timu yake kuzidiwa katika safu ya kiungo iliyowakosa Hassan Dilunga na Mrwanda Haroun Niyonzima ‘Fabregas’ ambao ni wagonjwa.
Vikosi vilikuwa:
Yanga SC: Barthez, Twite, Joshua, Rajab Zahir, Cannavaro, Said Juma, Msuva, Telela, Tambwe, Sherman na Coutinho/ Javu (dk 65).
Coastal Union: Kado, Hamis Mbwana, Athuman Tamim, Abdallah Mfuko, Tumba Lui, Abdulahim Humud, Joseph Mahundi/ Mohd Mtindi (dk 66), Godfrey Wambura, Hussein Sued, Rama Salim na Itubu Imbem/ Kenneth Masumbuko (dk 58).
CREDIT:SHAFFIHDAUDA
No comments:
Post a Comment