Advertisements

Wednesday, March 4, 2015

AENDA JELA KWA KUWAHI KUFIKA KAZINI MAPEMA

Kevin McGill anatarajiwa kwende jela wiki 14.

Mwendesha lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la Georgia nchini Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.

Kervin McGill yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua usumbufu kwa wengine na majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.

Kesi hiyo imewasitua watu wengi na kuchukua headline kwenye vyombo vya habari huku wengi wao wakiwa wameshikwa na mshangao wa mtu kwenda jela kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. Mtu kama huyu alistahili kupata onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.

3 comments:

Anonymous said...

mmmm jamani majuu ni majangaz,ije basi hii sheria na bongo yetu kwani kuwa watu wanasumbua watu sana heri na huyu alikuwa kwenye usafi wa taifa lake lkn ndio hivyo

Anonymous said...

On this land it is about "RULE OF LAW" and not doing the right thing or something right. Hayo mambo peleka bongoland

Anonymous said...

wazungu wanajipenda bwana hawataki kusumbuliwa hata kama unafaja wajibu wako kimahiri.ukikaa mitaa yakiswahili ndo hawa jamaa wanaweza kufanya mambo kama haya because watu weusi hawajaliwi sana,misnow inajaa mitaani mwao,polisi ukipiga simu haji haraka hata ebulesi so wache aende jela asike adabu zake.

mleteni bongo atafanya anavyotaka na kujisikia.

kuna nyoka makengeza wako above the law na nshomile anayetumia bilioni 10 kununua mboga wakati wako wananchi maskini hata mlo mmoja kwao ni SHIIIIIIIIIIIIIIIDAAAA.