Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete katika picha hii ya maktaba anaonekana akimpa hongera mama ambaye amejifungua salama yeye na mtoto wake. Afya ya mama na mtoto ni moja ya ajenda ambayo inapewa umuhimu wa pekee katika duru ya Jumuiya ya Kimataifa. Tanzania na Canada kupitia wakilishi zao za Kudumu katika Umoja wa Mataifa zimeanzisha kundi la Nchi Marafiki kuhusu ajenda hiyo ya Afya ya Mama na Mtoto lengo kuu kuhakikisha kuwa mama na mtoto ni ajenda ambayo haifi.
Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Gillermo Rishechynski (pichani) mapema wiki iliyopita waliitisha kikao cha kwanza cha Nchi Marafiki kuhusu afya ya Mama na Mtoto, kikao hicho cha kwanza na ambacho kilifanyika katika uwakilishi wa Kudumu wa Canada, kilijadili pamoja na mambo mengine dhumuni la kuundwa kwa kundi hilo ambalo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba afya ya mama na mtoto inaendelea kupewa umuhimu katika malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015, pamoja na kushawishi uwajibikaji na uwekezaji katika eneo hilo. kundi hilo linaundwa na nchi 40 kutoka mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea
Na Mwandishi Maalum, New York
Kundi la Nchi Marafiki kuhusu afya ya mama na mtoto limekutana na
kufanya kikao chake cha kwanza na kukubaliana kwa kauli
moja kwamba mama anapokuwa na afya njema anakuwa na uhakika
wa maisha yake na maisha ya mtoto wake.
Kama
hiyo haitoshi kundi hilo la nchi marafiki na ambalo
limekutana nchi ya uenyekiti-
wenza wa Wakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa
Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na
Balozi Gillermo Rishchynski, limekubaliana haja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa ajenda
kuhusu afya ya mama na mtoto inaendelea
na kubaki kuwa moja ya vipaumbele vya malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015
Kundi
la nchi hizo marafiki kuhusu afya ya mama na mtoto , linaundwa na wawakilishi kutoka nchi 40 zilizoendelea na zinazoendelea. Kikao
hicho kwanza, kimehudhuriwa pia maafisa
wa ngazi za juu kutoka Ofisi ya Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwamo Bi.
Amina Mohammed ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi na Mshauri wa
Katibu Mkuu, kuhusu Mipango ya Maendeleo
baada ya 2015.
Akizungumza
mwanzoni mwa kikao hicho Balozi Tuvako
Manongi amesemea, Tanzania imekubali
na inajisikia fahari kuwa mwenyekit- wenza wa kundi hilo, kutokana na ukweli kwamba, Idadi kubwa ya
vifo vya akina mama vitokavyo na matatizo ya uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga vinatokea
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
“
Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ni wadau wakubwa katika kulikabili tatizo hili
kwa kushirikiana na wadau wengine, tumepiga hatua za kuridhisha katika kuhakikisha kwamba mama mjazito hapotezi
maisha yake wakati wa kujifungua au mtoto mchanga hapotezi maisha yake mara tu
baada ya kuzaliwa ingawa changamoto bado ni nyingi”
Na
kuongeza kuwa juhudi hizi zinahitaji pamoja na mambo mengine
uwajibikaji wapamoja, uwezeshwaji
wa raslimali fedha lakini kubwa zaidi utashi wa kisiasa na
utimizwaji wa ahadi zinazotolewa na wadau mbalimbali.
Aidha
Balozi Manongi amesisitiza pia umuhimu wa elimu kwa wanawake na hasa watoto wa kike kwa kile anachosema,
mtoto wa kike akielimishwa kwa maana ya kupata fursa ya kwenda shule na
kusoma, anakuwa na uelewa mpana wa mambo
mbalimbali yakiwamo yanayohusu afya yake
mwenyewe lakini pia afya ya mtoto wake.
“
Elimu kwa wanawake na watoto wa kike, ni jambo muhimu sana, na hasa ikizingatiwa wanawake ndio uti wa mgongo wa Bara la Afrika, mwanamke na mtoto wa kike
anapopata fursa ya kupata elimu anao mchango mkubwa kwake mwenyewe, kwa familia
yake na kwa jamii inayomzunguka”
amesisitiza Balozi Manongi.
Naye
Balozi wa Canada, Gillermo Rishchynski,
pamoja na kusisitiza ushirikiano baina ya
wadau mbalimbali katika jitihada
hizi za kuimarisha kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. Amesema serikali yake imetenga dola za kimarekani 3.5bn kwa pindi cha 2015-2020 kwaajili ya afya ya mama na mtoto.
Kundi
la Nchi Marafiki kuhusu afya ya mama na mtoto litakuwa linakutana kila baada ya
wiki sita au nane na litajielekeza Zaidi katika katika kufanya tathimini ya hali ya sasa ya
utekelezaji wa malengo namba nne
na tano ya maendeleo ya millennia
mabayo utekelezaji wake unafikia ukingoni mwishoni mwa wamaka huu.
Kundi
hili pia litakuwa na fursa ya
kujadiliana, kubadilishana mawazo
pamoja na kujiwekea mipango ya namna gani ya kuongozea jitihada za
kusukuma mbele ajenda hii ya afya ya mama na mtoto kwa dhumuni la kupunguza
vifo vitokanavyo na uzazi, vifo vya
watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano.
Mwezi
Mei mwaka 2014 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper ambao ni wenyeviti wenza wa Kamisheni ya
Habari na Uwajibikaji kuhusu afya ya
mama, mtoto mchanga na mtoto waliongoza huko Toronto Canada, mkutano maalum wa wakuu wa nchi ambapo
ilikubalika kwamba suala hilo lipewe kipaumbele katika kukalimisha Malengo
ya Millennia yanayofikia ukiongoni mwaka
huu.
Ni
katika mkutano huo, ambapo ilikubalika
kwamba Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa
waunde kundi la nchi Marafiki kuhusu
afya ya mama na mtoto.
No comments:
Post a Comment