Injini ya treni almaarufu kama kichwa cha treni kikiwa nje ya njia yake (reli), jirani na machinga complex, barabara ya Kawawa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Machi 27, 2015, baada ya kulibamiza lori lililokuwa na shehena ya ngano mali ya kampuni ya Nyati. Dhahma hiyo ilitokea mapema asubuhi, lakini hadi inafika saa nane mchana, bado shughuli ya kukirejesha kichwa hicho kwenye nia yake ilikuwa pevu ambapo muda wote huo barabara ya Kawawa kutoka machinga compelex hadi kwenye mataa ya kuongozea magari barabara ya Chang'ombe na Nyerere ilikuwa imefugwa na kusababisha foleni isiyo ya kawaida
Winchi ya shirika la reli Tanzania (TRL), likiwa katika harakati za kukinyanyua kichwa hicho cha treni
Foleni iliyosbabishwa na ajali hiyo ambayo ,mashuhuda wanasema haikuleta maafa
K_VIS BLOG
No comments:
Post a Comment