Tuesday, March 24, 2015

AKATI WAGOMBEA WENGINE NDANI YA CCM WANA MLALAMIKIA LOWASSA HEBU TUJIULIZE HAYA MASWALI....

January Makamba amechapisha vitabu vyake
na kugawa kwa wajumbe wote wa mkutano
mkuu, mbona Lowassa hakulalamika?
January Makamba alinunua Simu za Gallaxy
Sumsang zaidi ya 140 akazigawa kwa wajumbe
wa baraza UVCCM ZANZIBAR.
January 2013 alipokusanya marais wa vyuo
vikuu Tanzania nzima Mt. Uluguru Hotel na
kuwalipa laki moja na nusu kila moja ili watoe
tamko kuwa anafaa kuwa rais, mbona Lowassa
hakulalamika?
Membe amekuwa akipendelea Wafuasi wake
kwenda kusimamia chaguzi Kama waangalizi
wa Sadc, mbona Lowassa hajalalamika?
Membe kanunua mabasi kwa baadhi ya
makanisa, mbona Lowassa hakulalamika...?
Membe amekuwa na kawaida ya kuplant
wagombea kama strategy yake na kuingilia
Chaguzi nyingi kanda ya ziwa mbona Lowassa
hajalalamika...?
Membe alipohudhuria tamasha la wasanii
Mwanza na tamasha la extra vaganza (la
wasabato) na kujipigia upatu mbona Lowassa
hakulalamika?
Mwigulu alikuwa akitembea na mabango ya
kuonyesha watu wakimuomba agombee mbona
Lowassa hakulalamika...?
Mwigulu pia kaandika mawe karibu yote kila
barabara TZ nzima mbona Lowassa
Hajalalamika...?
Na mwandosya pia amekuwa akitumia
Wanafunzi wa Vyuo Vya Mbeya na juzi
wamemuombe agombee Mbona Lowassa
hajalalamika...?
Mbona Pia Prof Muhongo anaombwa na umoja
wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Kilimanjaro,
Arusha na Kanda ya Kaskazini mbona Lowassa
hajalalamika.?
Sumaye mwezi december alipozunguka
makanisa yote, Mbeya, Dar, na Mwanza kwa
ajili ya kujitangaza mbona Lowassa
hakulalamika?...

1 comment:

Anonymous said...

Mbona Lowasa hakulalamika? Hii ndiyo lalama yake basi!!!