Advertisements

Saturday, March 21, 2015

CCM YAITIKISA ARUSHA MJINI KINANA NA NAPE WAAHIDI KURUDISHA CHAMA KWENYE MSTARI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Arusha mjini kwenye uwanja wa mkutano wa Sheikh Amri Abeid ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM itaendelea kuwatetea watu masikini na itahakikisha inawapa nafasi za uongozi watu wanaokubalika na wananchi.
 Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Onesmo Ole Nangole akihutubia wananchi wa Arusha ambapo aliwataka mawaziri kufanya ziara vijijini badala ya kukaa maofisini.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Arusha mjini na kuwaambia pesa isitumike kununulia madaraka .

 Amani Ole Silanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na kujiunga na CCM akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

  Amani Ole Silanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na kujiunga na CCM akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo alisema Chadema hakina watu wenye sifa za kuongoza.
 Aliyekuwa Mwenezi wa Chadema kata ya Olorien  Prosper Mfinanga (kulia) akionyesha baadhi mabango kwa Katibu wa NEC Itikadi wa CCM Taifa Nape Nnauye, Mwenezi huyo wa Chadema amejiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimia wananchi kabla ya kuanza kuhutubia wananchi,
 Prosper Mfinanga aliyekuwa Mwenezi wa Chadema wilaya ya Olorien akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kujiunga na CCM.
 Wananchi wakifuatilia mkutano
 Waandishi wa habari wakihakikisha wanapata kila tukio
 Umati wa watu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Sheikh Amri Abeid tayari kuhutubia.
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha Robinson Meitinyiku akihutubia wananchi wa mkoa wa Arusha ambapo aliwaambia wananchi hao Kikwete amerahisisha miundo mbinu, ameongeza vyuo na shule za sekondari na za msingi ,ameboresha huduma ya afya ikiwa ndio tafsiri ya maisha bora kwa kila mtanzania.

3 comments:

Nicky Mwangoka said...

Wakisema CCM nambari wani, wapo sahihi usiumie roho. Wanawajibika ipasavyo japo ambao hawapendi kuwa watu wa shukrani hawalioni hili.

Anonymous said...

Tatizo letu CCM ni kutawaliwa na rushwa hadi kwenye uchaguzi zote nchini. CHama na uongozi mzima imekuwa kazi kununua watu kutoka kwenye vyama vya upinzani!!Na kama ni kwe;li mbona hatujaona anayerudisha kadi toka TLP,CUF,SAU AU nCCR INAKUWAJE NI CHADEMA TU!! Huu ni ujanja mkubwa sana wa CCM na maneno ya kejeli yote yanayotolewa ni kwa ajili ya CHADEMA tu!!! Nadhani waTanzania kwa ujumla umefikia muda wa kutambua pumba na mchele ni upi la sivyo tutaendelea kutafunwa tuu na kuendeleza mikataba hewa ile ya nyuma inatendelezwa. Tunaomba ile fedha ya Escrow mliyogawana muirudishe kwanza mko wengi hadi kwa ..ba..a mwenye nyumba.

Anonymous said...

Wewe pigana na key bord ccm iyooo wache wale kwanza wakila unaumia ungepewa wewe mgao wa escrow ungekataaa ??mavi cha mkosaji