Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akiwa na wajumbe kutoka Zanzibar waliohudhuria mkutano wa 59 wa CSW
Anna Maembe, Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akifuatilia hitimisho la Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake. Nyuma yake ni Mhe. Jaji Angela Kileo
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia uhitimishwaji wa Mkutano wa 59 wa CSW
Na Mwandishi Maalum
Mkutano wa 59 wa
Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake umemalizika kwa kutoka na maazimio
mbalimbali likiwamo linalobainisha kuwa tofauti zote za usawa wa kijinsia zinamalizwa
ifikapo mwaka 2030
Mkutano huo wa wiki
mbili na ambao umehudhuriwa na mamia ya wawakilishi
kutoka mataifa ambayo ni wanachama wa
Umoja wa Mataifa, Taasisi za UM na Asasi zisizo za Kiserikali pia ulipitisha kwa kauli moja tamko la kisiasa ambalo limeainsha na kuazimia mambo kadha kwa kadha
yanayohusu fursa sawa za kijinsia na uwezeshaji wa mwanamke.
Ujumbe wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu,
uliongozwa na Mhe. Sophia Simba ( Mb), Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto.
Kupitia mkutano huo
wajumbe hao walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu
mafanikio katika utelekezaji wa
maazimio mbalimbali yaliyokubalika wakati
wa Mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995 pamoja na changamoto zake.
Akihitimisha mkutano
huo Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi na
Mkurugenzi Mtendaji wa UN- Women,
Bibi. Phumbzile
Malambo-Ngacuka amesema mwaka 2030 lazima uwe hitimisho la utofauti wa kijinsia
jukumu linalotakiwa kufanyiwa kazi
kuanzia ngazi ya familia, kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Naye Mwenyekiti wa
Kamisheni Bi Kandra Vajarabhaya
akizungumzia mwenendo mzima wa
mkutano huo anamesema, kwa wajumbe
kupitisha kwa kauli moja tamko la
kisiasa, kamisheni hiyo imerejea
wajibu wake wa
kuchagiza na kufanikisha
upatikanaji wa fursa sawa za kijinsia, uwezeshaji wa wanawake pamoja
na kuhakikisha haki za wanawake na
watoto wa kike.
Akatoa pia tathimini ya utekelezaji wa maazimio
pamoja na Jukwaa la utekelezaji
wa mkutano wa Beijing pamoja na changamoto
zilizobakia.
Kupitia mchakato
huu Bi
Vajarabhaya amesema wajumbe wamemejifunza
kwamba bado kuna changamoto , na
kwamba mkutano wa kamisheni hiyo
umetoka na mapendekezo kadhaa ya
kuimarisha utendaji wa chombo hicho.
Pamoja na majadilianao ya ajenda mbalimbali mkutano huo
umepitisha maazimio manne
likiwano linalohusu namna ya kuwasaidia wanawake wa Palestina, azimio hilo
lilipitishwa kwa kupigiwa kura ambapo kura 27 ziliunga mkono azimio hilo
huku mbili ( Israel na
Marekani ) zikilipinga.
1 comment:
Hivi kumbe kuna kibao cha Zanzibar huko Umoja wa Mataifa? Sasa mbona katiba haijayaweka haya sawa? Ama vipi?
Post a Comment