ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 12, 2015

CHIKAWE AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI 900 WILAYA YA NACHINGWEA KUJENGA MAABARA SHULE ZA SEKONDARI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololet Mgema msaada wa mifuko 900 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Maabara za Shule za Sekondari wilayani humo. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika mjini Nachingwea leo
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Michinge Mchopa akionesha sehemu ya msaada wa mifuko ya sarufi 900 iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Mathias Chikawe (hayupo pichani) kwa ajili ya ujenzi wa Maabara ya Shule za Sekondari wilayani Nachingwea. Waziri Chikawe alimkabidhi Mkuu wa Wilaya hiyo, Pololet Mgema (hayupo pichani) mifuko hiyo mjini Nachingwea leo. Picha zote na Felix Mwagara.

1 comment:

Anonymous said...

Sera za kutafuta ulaji kwa uchaguzi ujao watanzania tunadangantwa kweli akioata imetoka atajenga zake nne kwanza baada ya miaka mitano mtamsikia tena!