Dennis Ssebo akipanga mikakati kati ya EFM Redio na Raisi wa WBF Bwana Howard Goldberg pamoja na Francios Botha.
Dennis Ssebo akipanga mikakati kati ya EFM Redio na Raisi wa WBF Bwana Howard Goldberg pamoja na Francios Botha.
Francios Botha pamoja na Raisi wa WBF Howard Goldberg katika mazungumzo ndani ya kipindi cha Sports Headquaters.
Kutokana na mchezo wa ndondi kukua kwa kasi, kituo cha redio cha 93.7EFM kimeamua kusaidia kukuza zaidi mchezo wa ndondi nchini. Akiupokea msafara uliotoka Afrika ya Kusini na China, Mkuu wa Mahusiano wa ndani wa 93.7 EFM Dennis Ssebo,alisema muda umefika kuendelea kuunga mkono vipaji vya ndani.
“Tumeshazungumza na tumekubaliana mbinu mbali mbali za kuendelea kuinua mchezo huu,na ni mikakati gani tutatumia kuendelea kuiweka bendera ya Tanzania katika ramani ya kimataifa”,alisema Ssebo.
Mjadala mkali uliendelea katika kipindi cha Sports headaquaters cha EFM redio alipotua bingwa wa zamani wa masumbwi kwa uzito wa juu,Francious Botha akiwa na Raisi wa chama cha ngumi cha dunia cha WBF Howard Goldberg,kwa mahojiano na watangazaji wa kipindi hicho cha Sports Headquaters.
Nguli huyo wa masumbwi ambae ameshawahi kuzichapa na baadhi ya wakali katika masumbwi,Lennox Lewis na Mike Tyson,amewasili nchini akiwa na mkanda wa dunia wa WBF wa uzani wa Super Bantam utakaoshindaniwa na bondia Mohamed Matumla na Wang Xian Hua wa nchini China, siku ya Ijumaa tarehe 27 mwezi huu, katika ukumbi wa Dimond Jubilee.
Akizungumza katika studio zetu za EFM,Raisi wa chama cha ngumi cha dunia cha WBF Howard Goldberg,alisema kuwa Mohamed Matumla ambaye ni mtoto wa Rashid Matumla akionyesha kiwango cha kuridhisha,atapewa nafasi ya kuzichapa katika pambano la utangulizi katika hadhi ya dunia kule Las Vegas nchini Marekani baina ya bondia Floyd Mayweather na Mann Pacquiao litakalofanyika mwezi wa tano mwaka huu.
Botha au kwa jina lingine “White Buffalo” ,amewasili nchini kwa mara ya pili kwa mualiko maalum wa kampuni ya Hall Of Fame,inayo andaa mapambana ndani na nje ya nchi.Botha alitumegea kakipande tu cha taarifa,kwamba hapo baadae kuna pambambano linaandaliwa na litafanyika nchini Tanzania,ambalo litamshirikisha yeye na mmoja wa wakali wa kuzitwanga wa miaka hiyo,inawezekana ikawa ni Mike Tyson au Lennox Lewis.
Hata hivyo ,Afisa mtendaji wa Hall of Fame,bwana Jay Msangi,aliwahimiza watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kumshanglia Matumla Jr,wakati huo huo mpinzani wa Matumla Jr,Wang Xian Hua nae alishukuru EFM na Kampuni ya Hall of Fame,na watanzania wote kwa ujumla kwa ukarimu waliomuonyesha yeye pamoja na mkalimani na kocha wake walipotua tu nchini.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment