Tuesday, March 10, 2015

HILLARY CLINTON ASEMA ALIRUHUSIWA KUTUMIA BARUA PEPE BINAFSI

Hillary Clinton akijibu maswali ya waandishi habari leo ndani ya mjengo wa Umoja wa Mataifa New York kuhusiana na tuhuma za kutumia barua pepe binafsi badala ya serikali huku ikidhaniwa ni kwasababu alikua akificha jambo lakini yeye alipokua akiongea na wanahabari aliwaambia yeye kutumia barua pepe binafsi alomba kufanya hivyo na aliruhusiwa na sababu kubwa ya yeye kufanya hivyo ni kwasababu kwake ilikua vigumu kubeba simu mbili kwa ajili ya kutumia kupokea au kutuma barua pepe.

Alipoulizwa swali kama anajutia kufanya hivyo baada ya sasa wapinzani wake wanatumia kama mwanya wa kumshutumu, Hillary Clinton amesema anafikiria ingekua ni muafaka kama angetumia simu mbili wakati huo lakini sio siri  nimeisha watumia barua pepe zote za serikali na nimewaambia waziweke hadharani kila mtu aweze kuzipitia na kuona hazikua na siri kama watu wengine wanavyotumia mwanya huo kutafuta sababu ya kunikandamiza wakati mimi sio wa kwanza kutumia barua pepe binafsi kuna wenzangu walishafanya huko nyuma.

1 comment:

Anonymous said...

aliruhusiwa na nani kutumia hiyo barua pepe yake binafsi mbona Obama amestaajabu hayajui haya yeye.

lakini kwa kweli namkubali mwanamke huyu ni kichwa sana na wala hatetereke,mwanamke yeyote aliyesoma na kuelimika hatetereki na maisha wala shule.

mumewe alimletea zakuleta na vimada wake yeye naye akajisogezea kamzigo chake poa akawa anakula nacho na ndo maana akaambiwa jike dume because anatijambua.

namuombea mungu awe raisi wa marekani hizi habari wala hazimshtuwi anataka sana watu waziongelee kaenda shule huyu anajua anacho fanya sio mwanamke make up na wakurembua machooo na rege rege.