Advertisements

Saturday, March 28, 2015

JK atoa maagizo makali, ripoti ya CAG

Dar es Salam. Rais Jakaya Kikwete amekabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka unaoishia Juni 2014 na kuagiza vyombo vya dola kuwabaini maofisa wote wa Serikali wanaohusishwa na matumizi mabaya ya fedha za umma, ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Pia, Rais Kikwete ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa maofisa wote wa Serikali ambao wanahusika katika kulipa mishahara hewa kwa watumishi ambao wameacha kazi, wamefariki dunia au wamestaafu lakini wanaendelea kulipwa kupitia akaunti zao za benki.
Rais ametoa maagizo hayo jana baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na CAG Profesa Mussa Assad. Aliiomba ofisi hiyo kuisaidia Serikali kuboresha mfumo wa zabuni kwani Serikali inapoteza fedha nyingi kwa kupitia mchakato mrefu wa kupatikana kwa wazabuni wa kutoa vifaa na huduma kwa Serikali.
“Naagiza kuwa tutume ujumbe wenye nguvu za kutosha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Serikali.”
Ukaguzi huo umebaini upungufu mbalimbali katika usimamizi wa matumizi ya fedha za Serikali kama vile malipo yasiyokuwa na nyaraka, hati za malipo ambazo hazikuwasilishwa kwa ukaguzi, fedha iliyotumika nje ya bajeti, matumizi yasiyokuwa na manufaa na malipo ambayo hayakuidhinishwa na maofisa masuuli.
Profesa Assad amemweleza Rais Kikwete kuwa ofisi yake inapendekeza kuwa taasisi zote za Serikali zisiendelee kununua vifaa na huduma kutoka kwa wafanyabiashara wasiotumia mashine za stakabadhi za kielektroniki (EDF).
Kuhusu usimamizi wa rasilimali watu, Profesa Assad alimwambia Rais Kikwete kuwa ukaguzi wake umebaini kuwa mishahara ya watumishi waliocha kazi, waliofariki dunia na waliostaafu wameendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao.
Vilevile, fedha za makato ya mishahara ya wafanyakazi hao zimeendelea kupelekwa kwenye taasisi husika kama vile Bima ya Taifa ya Afya, Mamlaka ya Mapato na mifuko ya hifadhi ya jamii.”
Profesa Assad alisema tatizo hilo linaendelea kuwapo hata kama linapungua kwa sababu ya mfumo wa udhibiti ambao Serikali imeanzisha na kuwa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, mwaka 2014, kiasi cha Sh141.4 bilioni kilitumika kulipa watumishi hao hewa.
Mwananchi

4 comments:

Anonymous said...

Raisi wa Tanzania, Mhe Kikwete afuate mfano wa rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta: Watumishi wote wa Serikali waachishwe kazi papo hapo watakapojulikana kwamba wanafanya ifisadi. Wapewe hukumu kubwa sana kama mahakama inatagundua kwamba wamejeuka sheria za unongozi bora nchini. Kwanza, viongozi wote waliochukua escrow fund wachukuliwe hatua kali kama mfano wa uongozi bora. Pili, Hao wengine wadogowadogo nao wachukuliwe hatua kali sana.

Anonymous said...

Mambo ya baraza ya maadili hayo Chezea judge msumi kasheshe mji wa karimjee .Huyo Judge hilda gondwe mama Mkali yule jamani sijawahi ona alikuwaga katibu Mkuu pale afya oh mama alikuwa akiingia ofisini watu jii.Nilivyomuona kwenye hili baraza nikasema hapa watu jela watainusa .Kazi ipo mjini

Anonymous said...

Danganya toto miaka 10 wimbo ule ule. October ishia zako

Anonymous said...

CAG need to be independent, completely independent. Giving him additional responsibilities ndiyo kuendeleza rushwa na ksababisha CAG kushindwa kukagua without bias. Raisi, Washauri wako wako wapi??