Advertisements

Tuesday, March 31, 2015

KINONDONI MWENYEJI WA SIKU YA UPANDAJI MITI MKOA WA DAR ES SALAAM KESHO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko la wilaya hiyo kuhusu uzinduzi wa siku ya upandaji miti itakayofanyika kesho kimkoa eneo la Mabwepande wilayani humo. Kauli mbiu ya siku hiyo ni 'Panda Miti, Miti ni Hazina.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kupanda miti na kuitunza ikiwa ni kudumisha matumizi endelevu ya misitu kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Mwito huo umetolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondono, Paul Makonda ambapo alisema maadhimisho ya siku ya kupanda miti, kauli mbiu mbiu yake ni Panda Miti, Miti ni Hazina.

Makonda alisema lengo ni kuelimisha, kuhamasisha, na kuikumbusha jamii umuhimu wa kupanda miti ambapo kilele cha maadhimisho yatafanyika mkoa Dar es Salaam, wilaya ya kinondoni, katika shule ya msingi Mjimpya kata ya Mabwepnde.

"Kila mmoja wetu anafahamu kuwa miti ina faida nyingi kwa jamii yetu ikiwemo kutupatia matunda, kivuli, dawa za asili, mapambo, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, hewa safi, kuni, mkaa na mbao,".

Alisema misitu inahifadhi wanyama pori ambao ni kivutio kwa watalii wanaotupatia fedha za kigeni hivyo kila mmoja anawajibu wa kudhamini uwepo wa miti katika mazingira yake.

Aidha Makonda alisema miti ipandwe kwa mpangilio na kuzingatia ikolojia yake, na kuifanya hamashauri ya ya manispaa ya konondoni inakuwa na madhari nzuri na kuvutia.

Alisisitiza kuwa si vizuri kupanda miti mikubwa katikati ya barabara na karibu na nyaya za umeme, ambazo zinaweza kusababisha madhara hususan katika kipindi cha mvua.

No comments: