Advertisements

Monday, March 2, 2015

KUJIANDA NA MPAMBANO WA JUMAPILI KATI YA YANGA NA SIMBA PLUIJM ATIRIRIKA

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema wiki moja ya maandalizi kwa ajili ya Simba, itawasaidia sana.
Yanga inaivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara utakayopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Tayari Yanga iko kambini mjini Bagamoyo ambako ilipitiliza moja kwa baada ya kutua nchini ikitokea Botswana.
 "Pluijm amesema kuwa wiki moja itawasaidia kurekebisha makosa kadhaa.
“Makosa hayaishi katika mpira, lakini wiki moja ya maandalizi itatupa nafasi nzuri.
“Ukiona timu imecheza vizuri ujue mlichojifunza mmekifanyia kazi, mkishindwa kufanya vizuri utaona kuna sehemu mmepungukiwa.
“Soka ni lazima urudie kujifunza, leo, kesho na siku nyingine. Hivyo siku zaidi ya tano, zitasaidia kufanya marekebisho kwa maneno na mafunzo ya vitendo,”Mchezo wa mwisho kukutana timu hizi za Yanga na Simba ni kwenye Mtanini Jembe  na matokeo yalikuwa Simba kushinda goli mbili licha ya yanga kuwa bora kila idara lakini kwenye mchezo huo walilowa na kuwaacha wapenzi watimu hiyo ya jangwani wasiamini kilichotokea.
Mchezo wa Jumapili utavuta hisia za watu wengi kwani timu hizi zinavyokutana ni shida, home na kimuhemuhe kwa wapenzi wa pande zote mbili. Matokea mabaya ya pale zinavyokutana timu hizi makocha uwa na wakati mgumu wa kukosa ugali na watoto kuto kwenda chooni.

No comments: