Pichani ni Kadawi Limbu (kulia) akiwa na Samson Mwigamba
Shauri hilo ni namba 17 la Mwaka 2015, Katika Maombi yake kwa Mahakama Ndugu Limbu Anataka Mahakama Imzuie Mwigamba na Wenzie kujihusisha na ACT, Maombi Mengine nikutaka Mahakama kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mwishoni Mwa wiki hii.
Pia Limbu amenukuliwa akidai Kuwa Kwa Mujibu wa Katiba ya ACT-TANZANIA,Mwanachama anaweza kugombea uongozi ndani ya Chama hicho baada yakuwa Mwanachama kwa muda wa Miezi sita,
Pia amepeleka Shauri kwa Taasisi yakuzuia rushwa Nchini (TAKUKURU), akimlenga Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi kutokana na Jinsi alivyoshughulikia Mgogoro wa Chama hicho.
Habari za hivi Punde:
Leo mahaka imetupilia mbali pingamizi la Limbu aliyekuwa akiomba mahakama iweke zuio la mahakama kwa chama makini cha kizalendo kufanya mkutano mkuu.
Sasa ratiba ya chama itaendelea kama ilivyopangwa.....mkutano mkuu na uchaguzi wa taifa unafanyika tar.28...na uzinduzi rasmi unafanyika tar.29...matangazo yataendele kutolewa katika vyombo vya habari.
MABADILIKO
No comments:
Post a Comment