Advertisements

Thursday, March 19, 2015

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA WAMA NACHINGWEA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha waalikwa zawadi mbalimbali alizopewa ikiwemo chungu na mwiko, wakati wa sherehe za kutimiza mwaka mmoja za vikundi vya WAMA kwenye mradi wa mwanamke mwezeshe tarehe 18.3.2015. Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu Nachingwea, mkoani Lindi
Mama Kikwete akipungia wanavikundi wakati akiwasili kwenye sherehe hizo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mnacho iliyoko wilayani Ruangwa. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kukabidhi madawati 100 aliyowaahidi wakati alipozuru shule hiyo mwaka jana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti kwa Ndugu Fatuma Mchia, Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya WAMA Kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe kwa kuvuka lengo kwa kuingiza wanavikundi wengi kwenye mradi huo
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akianzisha mchango wa papo kwa papo kwa ajili ya Mradi wa Mwanamke Mwezeshe na kufanikiwsa kukusanya zaidi ya shilingi milioni moja.
Wanavikundi wakimsikiliza Mama Kikwete
Wanavikundi wakimsikiliza Mama Kikwete

No comments: