ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 28, 2015

MAMLAKA ZA MISHENI ZA ULINZI WA AMANI ZIWE WAZI-JENERALI MWAMUNYANGE

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa katika ukumbi wa Baraza la Uchumi la Umoja wa Mataifa maarufu kama ECOSOC ambapo ndipo ulipofanyika mkutano wa kihistoria wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi zinazochangia katika Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. Akichangia majadiliano ya mkutano huo. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amelishauri Baraza Kuu la Usalama na UN kuweka bayana na kwa uwazi mamlaka ya misheni inazoziunda. Pamoja naye ni Brigedia Jenerali MG. Luwogo na Brigedia Jenerali HS Kamunde.
 .Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyage akiwa ndani ya Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akibadilishana mawazo n mmoja wa Maafisa wa ngazi ya juu kutoka Idara ya Masuala ya Siasa katika UN muda mfupi kabla ya Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi hawajapiga picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 
Jenerali Davis Mwamunyange akiwa na ujumbe wake katika picha hii ambayo wapiga mbele ya bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku moja wa wakuu wa majeshi ya ulinzi kutoka nchi 108 kutoka kushoto ni Kanal Adolf Mutta, Brigedia Jenerali Luwogo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Mwamunyange, Brigedia Jenerali Kamunde, Meja Ngh'abi, na Luten Kanal Itang'are
" mnatuwakilisha vema?" ndilo swali ambalo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mwamunyange alilowauliza watanzania hawa wawili, Afisa wa Usalama wa UN Bw. Jacob Mwashiozya na Bw. Joseph Msami, wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipokuwa wakisalimiana naye na ujumbe wake mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiingia kwa staii ya aina yake wakati alipokwenda kufungua mkutano wa kwanza wa aina yake kufanyika katika Umoja wa Mataifa, ambapo Wakuu wa Majeshi ya ulinzi kutoka nchi zaidi ya 100 walikutana kwa wakati mmoja na mahali pamoja kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu operesheni za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa.

No comments: