ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 28, 2015

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC KUKAGUA MIRADI YA SHIRIKA MIKOANI

Mwonekano wa sasa wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Mlole Kigoma
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Ilembo Katavi. Nyumba hizo 70 zimeshakamilika na zinauzwa kwa wananchi wote wanaohitaji.Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na akiwa eneo la Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kukagua eneo ambalo ujenzi wa nyumba za gharama nafuu umeshaanza.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukikagua hatua ya ujenzi wa jengo la biashara la Paradise linalojengwa na NHC Mjini Mpanda kwa ajili ya shughuli za kibiashara
Mafundi wakiendelea na shughuli za ujenzi katika jengo la kibiashara linalojengwa na NHC eneo la Mpanda Mkoani Katavi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba sita za waalimu katika shule ya Kakuni Kibaoni Wilaya ya Mpanda msaada uliyotolewa na NHC ili kusaidia kuanza kwa shule hiyo. Picha hii imepigwa usiku baada ya msafara wa DG kufika katika mradi huo.
Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipoweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC katika eneo la Jangwani Mjini Sumbawanga.
Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na viongozi mbalimbali wakiondoka eneo la Jangwani baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukisikiliza maelezo ya ujenzi wa nyumba za gharama kwa kutumia teknolojia rahisi ulipotembelea kiwanda cha Saruji Mbeya kama sehemu ya kujenga mahusiano na kiwanda hicho ili kuwezesha ujenzi wa nyumba katika mikoa ya kanda ya nyanja za juu kusini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukioneshwa namna mashine ya Lafarge inavyotumika kuzalisha tofali za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ulipotembelea kiwanda cha Saruji cha Mbeya.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua ardhi ekari 285 inayomilikiwa na NHC eneo la Mwashiwawala Jijini Mbeya ulipofika kukagua eneo hilo.
Katika kuongeza utendaji wa kazi hususan uuzaji wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya nchini Mkurugenzi Mkuu wa NHC katika ziara zake mikoani amekuwa akikutana na Mameneja wa Mikoa wa NHC ili kila Meneja aeleze mikakati yake ya kuongeza mapato ya Shirika. Hapa ni kikao cha DG na Mameneja wa Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Morogoro na Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Isikizya Wilayani Uyui Mkoani Tabora

No comments: