Advertisements

Tuesday, March 3, 2015

MCHANGO WA SEKTA YA MADINI: TANZANIA IJAYO (2015-2035)

 Na Mwandishi wetu
Kwa sasa mchango wa Sekta ya Madini kwa Pato la Taifa (Tanzania) kwa mwaka (GDP by sector) ni 3.5%. Tukitaka kulinganisha hali ya uchumi wetu na ule wa nchi nyingine tunalazimika kutumia takwimu zinazopatikana ko kote duniani - za IMF, World Bank (WB) na African Development Bank (AfDB).

Pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka (GDP per capita) nchini Bostwana ni US$ 7,120 (IMF, 2013). Michango ya ki-sekta kwa GDP ya Botswana ni kama ifuatavyo: Sekta ya Huduma (Services, e.g. hotels, restaurants, transport, real estate, health, education) ni 62.4%, Viwanda yakiwemo madini (Industry) ni 35.7% na Kilimo (Agriculture) ni 1.9%. Kwa upande wa South Africa – GDP per capita ni US$ 6,621 na mchango ki-sekta ni kama ifuatavyo: (1) Services 65.9%, (2) Industry (yakiwemo madini) 31.6% na (3) Agriculture 2.5%. Jirani zetu Kenya: GDP per capita US$ 1,316 na mchango ki-sekta ni hivi – (1) Services 61.0%, (2) Agriculture 24.2% na (3) Industry (yakiwemo madini) ni 14.8%. Kwa upande wetu (Tanzania): GDP per capita ni US$ 719 na mchango ki-sekta ni kama ifuatavyo – (1) Services 47.9%, (2) Agriculture & Forestry ni 26.5%; Fishing 1.5% na (3) Industry and Construction (yakiwemo madini) ni 24.1%.

Takwimu za hapo juu zinaonyesha kwamba mchango wa Sekta ya Kilimo kwa Pato la Taifa la Tanzania (26.5%) ni kubwa kuliko la Kenya (24.2%), South Africa (2.5%) na Botswana (1.9%). Sisi (Tanzania) tuko chini sana kwa upande wa Sekta ya Huduma, ikiwemo Utalii (Services): Tanzania (47.9%), Kenya (61.0%), Botswana (62.4%) na South Africa (65.9%). Hapa tunalazimika kuongeza kasi ya kukuza Sekta hii muhimu kwa Pato la Taifa – suala hili litajadiliwa baadae. 

Takwimu za hapo juu zinaonyesha sisi wenye raslimali nyingi za madini bado tuko nyuma kulinganisha na nchi nyingine zilizofanikiwa kuwa na Pato zuri la Taifa kwa kupitia mchango wa raslimali za madini (ndani ya Sekta ya Viwanda, Ujenzi na Madini): Tanzania (24.1%), South Africa (31.6%) na Botswana (35.7%). 

Kwa Tanzania ijayo (2015-2035), Sekta ya Madini peke yake inapaswa kuchangia si chini ya 10-15% ya Pato la Taifa kwa mwaka. Mchango huu kwa Pato la Taifa ni muhimu uwepo ili kushirikiana na sekta nyingine za uchumi kama vile Sekta Ndogo ya Gesi Asilia (na baadae mafuta), na Sekta za Kilimo, Viwanda na Huduma ili kukuza uchumi wetu kwa zaidi ya 10% kwa mwaka kwa muda mrefu (kati ya miongo 2-3, yaani miaka 20 hadi 30) kwa nia ya kutekeleza uamuzi wetu wa kufuta umaskini kutoka nchi mwetu. Nini cha kufanya, kwa upande wa Sekta ya Madini kufikia malengo hayo? 2 

(a) Serikali kuwa na Hisa kwenye Migodi Mipya 

Serikali imefufua Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na lenyewe ndilo litakuwa na hisa kwenye migodi yote mipya itakayoanzishwa nchini. Prof Muhongo aliweka juhudi kubwa sana kulifufua Shirika hili na kuliagiza kazi kuu nne: (a) kupewa (baada ya majadiliano na makubaliano) na kusimamia hisa za Serikali (kwa niaba ya Watanzania wote) kwenye migodi mipya inayoanzishwa nchini. Kwa mfano Mgodi mkubwa wa Tanzanite wa Merelani, STAMICO ina 50% za hisa za mgodi huo. (b) Kuanzisha migodi yake yenyewe kwa niaba ya wananchi wote (Serikali) - mfano hapa ni Mgodi wa Dhahabu wa Tulawaka (STAMIGOLD), Biharamulo. (c) Kuwa mshauri na mwezeshaji mkuu wa Wachimbaji Wadogo na (d) Kuanzisha Kampuni ya kununua bati (tin) ya Kyerwa ili madini hayo yauzwe nje na sisi wenyewe (Tanzania) badala ya wachimbaji wa Tanzania kwenda kuyauza nchi jirani na nchi hizo kuyasafirisha ikiwa yanahesabika ni mali yao. Yote haya yanatekelezwa kwa mafanikio ya kuridhisha. 

MAPATO YA SERIKALI KUTOKANA NA MADINI YAMEONGEZEKA: Serikali kwa upande wake imepitia upya mikataba ya zamani ya madini ili kuongeza mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini nchini – hili linafanyika kwa mafanikio makubwa na wananchi wamefahamishwa kupitia njia mbali mbali za mawasiliano. 

(b) Wachimbaji Wadogo kuwezeshwa 

Prof Muhongo alipoanza kazi Mwezi April, 2012, alipanga na kuitisha kikao Dodoma (Juni 2012) cha Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo kutoka Mikoa yote nchini. Kikao hicho cha Dodoma kiliazimia yafuatayo: (i) Wachimbaji Wadogo waanzishe Vyama vya Umoja wao kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa - hili limefanyika. (ii) STAMICO iwe Mlezi, kwa vitendo, wa Wachimbaji Wadogo – kutoa ushauri wa kitaalamu wa utafutaji na uchimbaji wa madini, kuwasaidia kutayarisha miradi ya kupewa ruzuka na mikopo, kuwasaidia kupata vifaa ya uchimbaji madini, na kuwasaidia kupata masoko mazuri ya madini yao – haya yanafanyika, (iii) kuwapa mafunzo ya kutunza mazingira maeneo ya migodi yao – mafunzo yanatolewa, na (iv) Wachimbaji Wadogo kutoa ajira kwa vijana wetu, na kusaidia ukuaji wa biashara za kutoa Huduma (Services) kwenye maeneo ya migodi yao. 

(c) Wachimbaji wadogo kuwa Wachimbaji wa Kati 

Prof Muhongo amekuwa akisisitiza kwamba Watanzania wengi waingie kwenye uchimbaji wa madini kwa kuanzia ngazi ndogo hadi ile ya kati (mtaji wa US$ 20-100 Milioni) na kwenda juu zaidi. Serikali ilianza kutoa ruzuku ya US$ 50,000 mwaka jana (2014) na awamu ya pili (2015), itatoa ruzuku ya US$ 100,000 kwa kila 3 Kikundi/Kampuni. Ruzuku hizi zina lengo la kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo kupata mikopo mikubwa zaidi inayohitajika kwenye uchimbaji madini. 

Wachimbaji Wadogo ni kundi muhimu sana kama lilivyo kundi la Wachimbaji Wakubwa. 

(d) Tanzania kuanza kuchimba madini yanayohitajika kwenye teknolojia mpya za wakati huu na ujao 

Mbali ya kutegemea sana uchimbaji wa dhahabu na vito (k.m. almasi, tanzanite), Prof Muhongo aliagiza Geological Survey (Dodoma) ifanye utafiti wa madini ya aina ya REE (Rare Earth Elements) au Rare Earth Metals (k.m. lutetium, cerium, scandium, neodymium, europium, gadolinium) ambayo yanatumika kwenye utengenezaji wa vifaa vingi tunavyovitumia kwa wakati huu. Kwa mfano simu za mkononi (kwa sasa inakadiriwa kuna simu zaidi ya billion 7 zinazotumika ulimwenguni), kompyuta, TV, DVD, camera, rechargeable batteries, glass polishing, fluorescent lamps, alloys, lasers, fiber-optic, nk. 

Rare Earth Metals are essential to civilian and military technologies and to the 21stcentury global economy, including green technologies (e.g., wind turbines and advanced battery systems), medical technologies and advanced defense systems. The Japanese call them “the seeds of technology.” The US Department of Energy calls them “technology metals.” They make possible the high tech for the world we live in today. Haya madini yanapatikana Tanzania – ni ya thamani kubwa, tutayachimba na kuyauza. Tanzania ijayo (2015-2035) itapanua na kustawisha Sekta ya Madini ili ichangie si chini ya 10-15% ya Pato la Taifa letu. Document No. 3 Tarehe: 01 March 2015

No comments: