Chirstopher Mzazi katikaki akiwainua juu mabondia Julius Kisalawe kushoto na Said Uwezo kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumamosi ya march 28 utakaofanyika katika ukumbi wa manyara parck ccm tandale Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Julius Kisalawe kutoka Ndame Clab na Said Uwezo kutoka Mzazi GYM wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa utakao fanyika katika ukumbi wa manyara parck ccm tandale march 28 jumamosi
mpambano uho utakuwa chini ya oganaizesheni ya mchezo wa ngumi za kulipwa T.P.B.O ambapo msimamizi wa upimaji uzito Ibrahimu Kamwe alitoa taharifa kuwa bondia Uwezo alikuwa kazidi uzito na kumfanya apewe mda wa kukata uzito kwa masaa matano zaidi ili afikie lengo lake la kugombanmia ubingwa uho ambao unashikiliwa na Kisalawe
bondia huyo alikata uzito kwa mda unaotakiwa na kurusiwa kuwania ubingwa uho wa kg 52
mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kusindikiza mtanange uho ambapo bondia kutoka Super D GYM iliyopo shule ya Uhuru Vicent Mbilinyi atapambana na Yusuph Mkali mpambano wa raundi sita ambapo kiingilio katika mpambano uho ni silingi. 5000 tu na wanawake ni bule kabisa
siku hiyo kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa watu na mali zao
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment