Advertisements

Monday, March 2, 2015

PINDA ASHUHUDIA MLIMA WA MAHINDI AKIWA ZIARANI WILAYANI MBOZI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe, mama Tunu wakikagua sehemu ya shehena ya mahindi iliyohifadhiwa nje ya maghala ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula, NFRA, enjeo la Vwawa, wilayani Mbozi mkoani Mbeya Jumapili Machi 1, 2015. Maelfu ya tani ya mahindi, yamelazimika kuhifadhiwa nje baada ya maghala yaliyotengwa maalum kuhifadhi nafaka hiyo kujaa
Sehemu ndogo ya shehena ya mahindi yaliyonunuliwa na serikali na kuhifadhiwa nje ya maghara ya NFRA, Vwawa Mbozi baada ya maghala kujaa, Machi 1, 2015
Wasanii wakiwa wamejipamba nyuso zao
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Vwawa baada ya kufungua maabara zao akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015
Pinda akimuangalia msanii huyu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji WP Cecilia Mussa mmoja wa askari waliojeruhiwa akatika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Chang'ombe, barabara ya Mbeya- Chunya Machi 1, 2015. Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya na hali zao ni nzuri.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi na madaktari ya hospitali ya mkoa wa Mbeya wakati alipofika hospitalini hapo kuwaona majeruhi wa ajali ya askari wa kutuliza ghasia iliyotokea Februari 28, 2015 kati ya Mbeyana Chuna
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji WP Mwazanije Hassan mmoja wa askari waliojeruhiwa akatika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Chang'ombe kwenye barabara ya Mbeya Chunya Machi 1, 2015. Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya na hali zao ni nzuri
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimfariji WP Mwazanije Hassan 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wauguzi na madaktari wa hospitali ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi wa Vwawa , Mbozi akiwa katika ziara ya mkoa wa mbeaya Machi 1, 2015
Wasanii wakijipumzisha baada ya kazi kubwa ya kuburudisha na kuahmasisha
Pinda akisimikwa na wazee wa Vwaya

No comments: