ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 1, 2015

RATIBA YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU MHE. CAPT. JOHN KOMBA ITAKUWA KAMA IFUATAVYO:

Marehemu Kapteni Komba enzi za Uhai wake.


Kesho tarehe 02/3/2015 saa 1 asubuhi misa parokia ya Mt. Bikira Maria Mpalizwa iliopo mbezi , saa 4 asubuhi mwili utaelekea Karimjee kwa ajili ya kuagwa, na saa 8 mchana mwili utaelekea airport tayari kwa safari ya Songea. Mazishi yatafanyika tarehe 3/3/2015 kijijini kwake Lituhi.

Kufuatia Msiba huu shughuli za kamati hazitakuwepo kwa kesho tarehe 2/3/2015. Ukipata taarifa hii tafadhali mjulishe na mwingine.

IMETOLEWA NA;
OFISI KATIBU WA BUNGE
1.3.2015

No comments: