ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 2, 2015

SALAAM ZA POLE

John Komba enzi ya uhai wake

CHAMA CHA MAPINDUZI D M V MAREKANI Kwa niaba ya C C M Tawi la Washington DC Virginia na Maryland Tumepokea kwa mshtuko mkubwa sana habari za kifo za Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya C C M Mbunge wa Mbinga Magharibi na Msanii Maarufu Nchini Tanzania Marehemu John Komba 

 Kwabahati niliwahi kufanya kazi kwa karibu sana wakati akiwa kiongozi wa kikundi cha Sanaa cha Jeshi La Wananchi nami nikiwa kiongozi wa DDC kibisa ni Msanii hodari Mwenye kipaji kikubwa sana NchiniTanzania Taifa limepoteza Kiungo Muhimu sana kwenye Sanaa 

 Natoa salamu zangu za pole kwa wa C C M wenzangu kwa kuondokewa na mwanachama mwenzetu na mjumbe wa halmashauri ya Taifa Mbunge wa Mbinga magharibi Tunatoa pole kwa wananchi wote wa Jimbo la Mbinga Magharibi Wasanii wote Mashabiki wa Sanaa BASATA Wizara ya Utamaduni Ameacha pengo kubwa tunatoa pole kwa Mkewe Watoto Familia yote Wasanii Wote wa TOT Naomba Mwenye Enzi MUNGU Amweke Mahala pema peponi Amen SALMA MOSHI KATIBU ITIKADI NA UENEZI C C M D MV MAREKANI

1 comment:

Anonymous said...

Jamani habari humu ziwe zinafanyiwa editing. Tuheshimu kanuni za uandishi wa lugha fasaha. Tuliishakosolewa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alipokuja. Habari hujui sentesi zinaishia au kuanzia wapi. Hakuna Kituo wala koma! Vijimambo upo daraja ya juu sasa itabidi utafute mtu asaidie kufanya editing kabla hujatoa humu. Dunia nzima inasoma.