ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 5, 2015

TAMASHA LA WANAWAKE KUJA NA MABADILIKO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark (katikati) Agnes Mgongo (anayezungumza,wa pili kushoto) Elias Barnaba msanii (wa kwanza kushoto) na Anty Mandoza, mratibu mkuu wa warsha hiyo.
Bango lenye ujumbe wa Siku ya Wanawake Duniani.
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba, akizungumza namna atakavyowaburudisha wanawake siku hiyo.

WAKATI zimebaki siku chache kufikia kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, waratibu wa warsha hiyo, leo ameelezea kwamba patachukuliwa hatua za mabadiliko yatakayokwenda sambamba na maadhimisho hayo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mgongo aliwaomba wanawake wajitokeze katika maadhimisho hayo yatakayofanyika kitaifa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar akisema siku hiyo ni ya kipekee kwa mwanamke kupigania haki yake ya msingi katika kujikwamua kimaendeleo na kifikira.

Mgongo alisema mgeni rasmi katika hafla hiyo itakayoanza saa 10 jioni hadi saa 4 usiku, atakuwa mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda.

Miongoni mwa mambo yatakayofanyika siku hiyo ni mafundisho ya kupambana na changamoto kwa kuzibadilisha kuwa fikra.

‘’Ninawaombeni wanawake wenzangu mjitokeze katika ukumbi wa Mlimani City ambapo siku hiyo tutafundisha mbinu za kupambana na changamoto kwa kuzibadilisha kuwa fikra, ’’ alisema Mgongo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kingilio katika warsha hiyo kitakuwa ni Sh. 50,000 na Sh.30,000 kwa ajili ya meza ya maonyesho ya biashara na kwamba fedha zitakazopatikana asilimia 10 zitaelekezwa katika kuwaandaa wasichana kujitambua mapema kabla ya kuingia katika ajira.

(PICHA/STORI NA DENIS MTIMA/GPL)

No comments: