Advertisements

Thursday, March 5, 2015

NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA DELTA YAPATA AJALI UWANJA WA NDEGE LAGUARDIA NEW YORK

Ndege ya shirika la ndege la Delta leo AlhamisI March 5, 2015 imepata ajali ya kuteleza kwenye theluji ilipokua ikitua kwenye uwanja wa ndege wa LaGuardia wa New York, ndege hiyo iliyokua ikitokea Atlanta iliacha njia na kugonga uzio wa seng'enge ya waya kama inavyoonekana kwenye picha na msemaji wa zima moto ameripoti hakuna mtu aliyekufa kwenye ajali hiyo isipokua baadhi ya ya abiria wamepata majeraha ya kawaida na walikimbizwa hospitali kwa matibabu na kwa sasa uwanja huo umefungwa kwa ndege kuruka au kutua mpaka saa 1 usiku kwa saa za Amerika ya mashariki.
Abiria wakisalimisha maisha yao baada ya ndege ya shirika la ndege la Delta kupata ajali ilipoteleza kutoka kwenye njia yake kutokana na theluji inayoendelea kuanguka mapema leo.
Abiria wakitoka kwenye ndege kuokoa maisha yao

No comments: