ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 4, 2015

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KAMISHENI YA TAKWIMU YA UMOJA WA MATAIFA

Mkutano wa 46 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja ya Mataifa umeingia katika siku ya pili ambapo wajumbe wa Kamisheni hiyo wanajadiliana na kupitisha maazimio mbalimbali yanayohusia na masula ya kitakwimu katika maeneo mbalimbali.

Mkutano huu ambao ni wa siku nne unafanyika katika kipindi ambacho Jumuiya ya Kimataifa inaendelea na jukumu kubwa la kuaanda na kukamilisha rasimu ya malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs) mchakato ambao umekwisha ainisha jumla ya malengo 17 yamekwisha ainishwa.
Pamoja na wajumbe wa Kamisheni hiyo ambayo inaundwa na nchi 24, ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kati ya nchi tano za Afrika zikiliwakilisha Bara la Afrika, kujadiliana masuala mtambuka yahusuyo Takwimu pia wanajaliana na kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu wa nafasi ya Taasisi za Takwimu katika kuandaaa viashiria ( Indicators)vya malengo hayo 17.
Taswira ya washiriki wa Mkutano wa 46 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo wa siku nne, unaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Dr. Albina Chuwa ( mwenye suti ya damu ya mzee).

No comments: