Advertisements

Friday, March 6, 2015

TAWI LA CCM NEW YORK

Uongozi wa CCM New York na vitongoji vyake unapenda kutoa shukran zake za dhaki kwa moiyo ya kujitolea kwa hali na mali kwa watu wote waliohudhuria sherehe ya CCM kutimiza miaka 38 mjini New York.
Pia tunawashukuru wanachama wote na wasio wanachama kwa michango ilofanikisha shughuli hii na kuna wengine walichangia na hawakuja wote tunawashukuru.
Shukran za pekee zimwendee mgeni rasmi mh. Ridhiwani Kikwete kwa ushauri na mema yote aliyotufanyia hata kuja kujiunga nasi kwenye sherehe juu ya kazi nyingi na majukumu makubwa alionayo.
Mwisho tunapenda kuwashukuru watu wote hasa watanzania wenzetu waliochangia kwa namna moja au ingine kufanikisha sherehe yetu.
Tukumbuke umoja ni nguvu, pamoja tutaweza. 
Mwenyekiti Sefu Akida

No comments: