Dkt, Andrea Atzori akiwa na Bi. Tully Mwaipopo, Afisa wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mara baada ya uzinduzi wa onyesho hilo
Balozi Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akizungumza wakati wa uzinduzi wa onyesho la picha lililoandaliwa kwa ubia baina ya Wakilishi za Kudumu za Italia na Tanzania. Onyesho hilo linahusu huduma za afya ya mama na mtoto zinazotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Doctors with Africa CUAMM katika hospitali ya Tosamaganga, Mkoani Iringa. Kushoto kwa Balozi Manongi ni Balozi wa Italia katika Umoja wa Mataifa, Bw. Sebastioano Cardi na kulina ni mmoja wa Wabunge kutoka Italia anayehudhuria mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake
Balozi Manongi akiteta jambo na Dkt. Andrea Atzori ambaye katika maelezo yake amesema taasisi hiyo ya Doctors with Africa CUAMM inampango wa kupanua huduma zake katika maeneo mengine ya pembezoni mwa Tanzania, mbali ya Tosamaganga na Mikumi
juu na chini ni baadhi ya picha zinazoonesha huduma ya utoaji wa afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya Tosamaganga , huduma hiyo ainayoendana manafumzo kwa wataalamu wa afya imeweza kuokoa maisha ya wanawake wajawazito pamoja na watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda.
Na Mwandishi Maalum,
New York
Tanzania imeelezea
kuridhishwa kwake na ushirikiano uliopo
baina ya Serikali na Taasisi Binafsi katika
uboreshaji na utoaji wa huduma za
afya zikiwamo zinazomlenga mama na
mtoto. Na hivyo kuchangia katika upiguzaji wa vifo vya mama wajawazito na
watoto wachanga
Kauli hiyo imetolewa
siku ya jumatatu na Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati wa uzinduzi wa onyesho kwa njia ya picha kuhusu huduma za afya zinazotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Doctors with Africa CUAMM inayofanya
shughuli za utoaji wa huduma za afya ya
mama na mtoto katika Hospitali ya
Tosamaganga, Mkoani Iringa.
Picha hizo zinaonyeshwa katika corridor
za Umoja wa Mataifa, sambamba na mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Hadhi ya
Wanawake ( CSW) unaofanyika hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano unaojadili masuala mbalimbali
yanayomhusu mwanamke na mtoto wa kike, kuanzia elimu, fursa na haki sawa, huduma bora za afya, uwezeshwaji , haki za mwanamke na mtoto wa kike
pamoja na changamoto zinazo wakabili.
Balozi Manongi amesema
ni kwa kushirikiana ndipo nchi
kama Tanzania inaweza
kuongeza kasi ya kuwafikishia huduma za afya wananchi wengi, na kuwa uwepo wa Taasisi kama ya Doctors with Africa CUAMM na mchango wake katika utoaji wa huduma za afya
huko Tosamaganga na maeneo mengine ni
kielelezo sahihi cha ushirikiano
anaouzungumzia.
Akasema mchango wa Taasisi hiyo ni mfano wa kuigwa na ndiyo maana Tanzania katika maandalizi ya malengo mapya
ya maendeleo baada ya 2015 moja
ya maeneo inayoyapigia chapuo ni pamoja na hilo la afya ya mama na mtoto pamoja
na ushirikiano miongoni mwa wadau
mbalimbali.
“ Nyinyi ni kielelezo sahihi cha ubia na ushirikiano tunaouhimiza. Asanteni sana kwa mchango wenu
na asanteni kwa kudhirisha kwamba
inawezekana kufanya kazi kwa ushirikiano”. akasema
Balozi.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa Taasisi hiyo, Bw. Andrea
Atzori, amesema Taasisi yake ambayo
imekuwa nchini Tanzania tangu
mwaka 1968 imejielekeza Zaidi katika
utoaji wa huduma za afya katika maeneo ya
vijijini hususani kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga wakiwamo wanaozaliwa kabla ya muda.
Huduma nyingine zinatolewa na taasisi hiyo ni pamoja na mafunzo kwa wataalamu wa
afya, huduma za uzazi salama kupitia
mpango wao wa miaka mitano walioupa
jina la “mama na mtoto kwanza”.
Aidha kwa mujibu wa Dkt. Andrea Atzori, Taasisi hiyo inatarajiwa kupanua huduma zake
katika maeneo mengine Zaidi ya pembezoni
kwa lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata huduma ya afya pale
walipo.
Pamoja na
Tanzania, Doctors with Africa CUAMM
iliyoanzishwa mwaka 1950 na makao yake
yakiwa nchini Italia,pia inaendesha shughuli zake katika nchi za Angola,
Ethiopia, Msumbiji, Sudani ya
Kusini, Uganda na Sierra leone
1 comment:
tafakari kwa nini wageni wa kila aina wanakuja kutusaidia Tanzania na bara la Africa?wanatupenda sana,wanatuhurumia sana?wanatutakia mema?wanapata faida gani?
amka jitambuwe.
Post a Comment