Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 16/03/2015 hadi tarehe 12/04/2015. Aidha katika kata ya Utengule ya Mji mdogo wa Makambako Uboreshaji utafanyika kuanziatarehe 9-15/03/2015
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
RATIBA YA UBORESHAJI WA
DAFTARI LA KUDUMU NJOMBE – HALMASHAURI YA
MJI WA NJOMBE
|
|
UBORESHAJI
WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
MKOANI
NJOMBE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi
wote wa Mkoa wa Njombe kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric
Voters Registration” kuanzia tarehe 23/02/2015
hadi tarehe 01/03/2015
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji
na Mitaa.
Watakaohusika
katika zoezi hili ni wananchi wote:-
·
Waliotimiza
umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale wote watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
·
Waliojiandikisha
awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa
zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
·
Wale wote
ambao wanazo sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.
Zoezi litaanza kufanyika Wilayani Njombe katika
Halmashauri ya Mji Mdogo wa Makambako.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote
wa Mji Mdogo wa Makambako kujitokeza kwa
wingi kuanzia tarehe 23/2/2015
mpaka tarehe 01/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili
kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu
wa mwaka huu 2015.
Kumbuka:-
Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati
wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.
Tangazo
hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
|
|
UBORESHAJI
WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
MKOANI
NJOMBE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote
wa Mkoa wa Njombe,Halmashauri ya Mji mdogo wa Makambako kuwa itaanza zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya
“Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015 katika kata ya Kitisi, Kivavi, Lyamkena,
Maguvani, Majengo, Makambako, Mjimwema, Mlowa, na Mwembetogwa. Kata ya
Kitandililo utafanyika tarehe 03 -09/03/2015. Kata ya Mahongole tarehe
11-17/03/2015 na Kata ya Utengule uboreshaji utafanyika tarehe 19 – 25/03/2015.
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji,
Vitongoji na Mitaa
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi
wote:-
·
Waliotimiza
umri wa Miaka 18 na kuendelea
na wale wote watakaotimiza miaka
18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
·
Waliojiandikisha
awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa
zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
·
Wale wote
ambao wanazo sifa za kujiandikisha
lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari
Zoezi litaanza kufanyika Mkoani Njombe katika
Halmashauri ya Mji wa Makambako na Mji wa Njombe.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote
wa Mji Mdogo wa Makambako kujitokeza kwa
wingi kuanzia tarehe 23/2/2015
mpaka tarehe 25/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka huu 2015.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa
2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Kumbuka:-
Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati
wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.
Ruth Masham
Kny:
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
TEMBELEA
No comments:
Post a Comment