ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 12, 2015

Uliona alichoandika Naibu waziri wa fedha mh.Mwigulu Nchemba baada ya kupokea taarifa ya kufutwa uanachama Zitto Z.Kabwe

kulia ni Mb.Mwigulu Nchemba,katikati ni Mbunge wa Jimbo la Manyovu Kigoma Obama na anaefuata ni Mb.Zitto Z.Kabwe
Imenisikitisha sana,Nimesikia taarifa za kuenguliwa uanachama kwa Mh.Zitto Kabwe ndani ya Chama alichoanzia siasa,alichokitumikia kwa Jasho na mali,alichowekeza muda na akili yake kwa zaidi ya miaka 19.
Zitto amekuwa/anaendelea kuwachachu ya mabadiliko kwa Vitendo kwa Taifa letu.Uwezo wa kisiasa wa Kabwe adhabu yake sio kumfukuza,Demokrasia ni lazima itumike.

Nakusihi kijana Mwenzangu,Mwanasiasa Mwenzangu na Mchumi Mwenzangu kuwa,Taifa linakuhitaji sana wakati huu tunapopambana na ufanyaji kazi kwa mazoea na kuleta "MABADILIKO KWA VITENDO"Hivyo usikate tamaa watanzania watakuhesabia mema kwa yote unayoyafanya kwaajili ya Taifa letu. Mwigulu Nchemba

Chini hapa nimekuwekea twit za Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya kufukuzwa uanachama kwa Zitto Zuberi Kabwe

#Zitto Taifa linakuhitaji,Usikate tamaa


#Zitto Uwezo wako wa kisiasa,adhabu yake sio kuenguliwa.Ww ni hazina kwa Taifa


#Zitto Watanzania wanatambua mchango wako kwa Taifa,Wanakuhitaji usikate tamaa

3 comments:

Anonymous said...

Mheshimiwa saana, Ni vyema kabisa viongozi tukafanya kazi za wananchi walizotutuma au kuwajibika katika nafasi tulizopewa.! Kwanini? Hili jambo la kutimuliwa mheshimiwa Z. ni jambo la kawaida katika siasa na popote pale duniani!. Isitoshe limeamuliwa na mahakama na kama kulikuwako na mkono wa chama Tawala (CCM) basi ni udhaifu wa kisiasa. Mwigilu kwenye sakata la TEGETA Escrow na tena ukiwa naibu waziri umelikalia kimya sana badala ya kulivalia kidedea kama kiongozi wa kifedha! Na bado tunaendelea kusikia jinsi RUGEMALILA anavyo endelea kutamkwa na hadi leo hii hatujasikia ameitwa popote au kukamatwa. Hili za Zito linaonekana kushika kasi hata kabla yeye mwenyewe hajaweka maamuzi inaoanekana kuanza kumchumbia! Wako wanachama na viongozi wengi tu wa CCM wamefukuzwa au kusimamishwa! na hivyo la Zito lisiwe la kunganania kumsifu wakati huu mgumu kwake muacheni aamue mwenyewe. Hivi angekuwa kwenye chama chetu CCM na kufanya mambo kinyume na utaratibu wa katiba ya chama ulitarajia maamuzi yawe yapi katika kamati husika au jambo likishafika kwenye sheria! Au kwa kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu ndio basi tulifanye la kuingia kwenye mikutano ya kujinadi na kuviona vyama vingine havina utaratibu wa kikatiba unaowaweza kuendesha vyama kisheria na kimaadili!. Tuwe wakweli na kuheshimu taratibu za vyama husika kwani navyo vina utaratibu wa kisheria na utawala unaoweza kuimarika zaidi hata ya sisi!! Taratibu zipo zinatakiwa kufuatwa. tufanye kazi za wananchi sio kwenye malumbano na majukwaa ya kuvichafua vyama! Ingekuwa jambo laa maana sana serikali na vyombo vya sheria vikaliweka wazi swala la ESCROW na watuhumiwa wake, chama tawala kikishirikiana na vyama kulipitia daftrari la wapiga kura, katiba iliyotarajiwa isingananizwe kupitishwa kwani hadi hii leo hakuna elimu tosha kwa wananchi inasubiriwa kuipachika kwamba imepita kama inavyopigiwa kuw aitapita tuu HOW?/ It is IMPOSSIBLE tusije leta mapigano!! Mwisho swala la Zitto liachwe kama lilivyo yeye mwenyewe anajua chama gani aende.. NUKTA.

Anonymous said...

Asante sana mh. Mwigilu. Hapa sasa itakuwa dede la kubebana na swala zima la Zitto kwenye magazeti, vikao, mikutano kwani Chama chake si kina utaratibu sawa na chama cha CCM mwanachama akienda kinyume na utaratibu anaadhibiwa kuendana na katiba sasa hapa kuna kosa gani isitoshe mahakama iliamua ilivyoona! Anaweza kurudi na kwenda kuomba samahani ikaisha akaendelea kuwa mwanachama wa kawaida kwa muda fulani iko shida gani??

Anonymous said...

Tatizo kubwa lililopo kwenye siasa uchwara hasa ya Tanzania ni kutoelimika katika maswala nyeti. Mambo mengi viongozi wetu wanasubiri tukio fulani ndio wawajibike. Mfano mzuri ni uchaguzi unaotarajiwa waone viongozi wanavyotoa misaada kwani walikuwa wapi hali zimewatatiza sana wananchi waliowaweka madarakani katiba yenyewe wameshindwa kuitizama vyema na kuweka matakwa na masilahi yao mbele! Kwani lazima tuendelee na alichotaka Muasisi JKNyerere??!!- Twende na wakati na sheria zifuate mikondo yake. Swala la Zitto sio la kuuzia magazeti na kumfuata kila awapo. Na ndugu yangu Zitto usipende kudalaliwa maamuzi unayo mwenyewe. Hii chama yetu ya CCm unaijua ilivyo kama ulishakuwa mpinzani na ukiamua kukaa nao meza moja shauri yako wanajua jinsi ya kuwanyamazisha watu!! Kaaa mbali ndg yangu. Wako vibobea!!. Asante