Mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo Media Krantz Mwantepele akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kituo cha wazee wasiojiweza Msimbazi kinachosimamiwa na jimbo kuu hapa dar es salaam kanisa la katoliki na kuhudumia wazee wapatao kumi na moja waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu.Timu nzima ya Mwanaharakati Mzalendo Media ilikuja hapa kuwaona wazee hawa na kupata nafasi ya kuwafariji na kutoa baadhi ya misaada ya chakula na nguo za kuwasitiri leo siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Mdau Marko Mlonganile akipata nafasi ya kumsalimia mmoja ya wazee wanaopatikana katika kituo hiki na kupata nafasi ya kujua baadhi ya changamoto zinazopatikana katika kituo hiki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Mdau subilaga james akiwa katika taswira na mmoja bibi wanaopatikana katika kituo hiki cha wazee wasiojiweza kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam la kanisa katoliki na kuweza kuhudumia wazee wapatao kumi na moja
siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Bibi ambaye ni mmoja ya wazee wanaotunzwa katika kituo hiki akitabasamu baada ya wadau wa Mwanaharakati Mzalendo Media kutembelea hapa na kuweza kuwafariji kwa kukaa nao na pia kutoa mahitaji kwa ajili ya chakula na nguo za kuwasitiri katika kituo cha wazee wasiojiweza hapa jijin dar es salaam kituo kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam katoliki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Bibi akitabasamu baada ya wadau wa Mwanaharakati Mzalendo Media kutembelea hapa na kuweza kuwafariji kwa kukaa nao na pia kutoa mahitaji kidogo kwa ajili ya chakula na nguo za kuwasitiri katika kituo cha wazee wasiojiweza hapa jijin dar es salaam kituo kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam katoliki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Baadhi ya wadau toka Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakiongea na mmoja ya wazee aliyelala kitandani ni moja kati ya wanaotunzwa na kituo cha wazee siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Moja ya nyumba ambayo inatunza wazee wasiojiweza na ni kituo kinachosimamiwa na kanisa katoliki jimbo kuu dar es salaam
Mahojiano yakiendelea na msimamizi wa kituo hiki sister angelina hapa akieeleza historia fupi ya kituo na jinsi wanavyowahudumia wazee katika kituo hiki
Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media Krantz Mwantepele akitoa maelezo kidogo kwa msimamizi wa kituo hiki sister angelina (hayupo pichani ) na wanaosikiliza kwa makini ni wadau Subilaga na Happy
Wadau wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakifurahi jambo na msimamizi wa kituo hiki sister angelina
Tukikabidhi baadhi ya michango kama mahitaji muhimu ya chakula kwa mismamizi wa kituo cha wazee wasjiojiweza sister angelina anayeshuhudia ni mdau bensoni
Mmoja wa wazee akiongea jambo mdau Marko mlonganile huku mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo media Krantz Mwantepele akisikiliza kwa makini .
Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media krantz mwantepele akikabidhi baadhi ya misaada ya chakula na nguo kwa msimamizi wa kituo hiki siter angelina iliyotolewa na wadau wa mtandao wa Mwanaharakati mzalendo Blog
Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA Krantz Mwantepele akiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki baada ya kumaliza safari ya kuwaona wazee katika kituo hiki na kutoa baadhi ya mahitaji ya chakula na nguo za kuwasitiri
PICHA ZOTE NA ALFRED MLONGANILE
No comments:
Post a Comment