ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 29, 2015

Wanakwaya Wamfungukia Jokate, Wadai Anatia Aibu



Mrembo , mtangazaji na muigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewakera wanakwaya wenzake ambao wamedai kuwa anawatia aibu.
Kwa mujibu wa gazeti la Ijumaa, ishu ya Jokate kutupia picha za nusu utupu mitandaoni si mpya, mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kwa tabia yake hiyo kiasi cha kuwakera wanakwaya hao wa kanisa analosali la Saint Peter lililopo Oysterbay jijini Dar.
Mbali na picha hizo, safari hii anaandamwa na skendo mpya ya kudaiwa kukata mauno mbele ya midume anapokuwa kwenye shoo zake baada ya kutumbukia kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Kwa mujibu wa baadhi ya wanakwaya hao, wamekuwa wakimjadili mara kwa mara hasa wanapokuwa mazoezini kanisani hapo mara baada ya mmoja wao kurushiwa picha za mwanadada huyo kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wanakwaya hao walikwenda mbele zaidi na kudai kwamba mbali na kuwa ni kioo cha jamii lakini bado ni alama ya kanisa hivyo ni aibu kwa kanisa pia kwa sababu binti aliyelelewa kidini kama Jokate hawezi kuwa na tabia za aina hiyo.

Kuna baadhi walidai labda mwanadada huyo anafanya hivyo ikiwa ni njia ya kujitangaza yeye na biashara yake bila kujali kama anaweza akajiondolea ute wake na heshima aliyoijenga kwa miaka mingi.
“Ukweli ni kwamba Jojo (Jokate) anatutia aibu maana malezi ya kidini hayapo hivyo. Anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watu wote.

“Sisi tunamshauri arudi awe kama zamani kwani alikuwa binti wa mfano kanisani. Hakuna mtu wa kuonesha maumbile yake muhimu hadharani. Kwanza alipoingia kwenye mambo ya muziki ndiyo hali imekuwa mbaya maana ukiona video zake hutamani kuziangalia na watu wenye heshima zao,” alisema mmoja wa wanakwaya hao kwa niaba ya wenzake huko akiomba chondechonde kutotajwa na gazeti hilo.

Mwingine akasema: “Unajua Jokate niliyekuwa namjua mimi siyo huyu, siyo huyu wa kupiga picha hizi chafu, kwa kweli ni aibu kwake na kwetu pia kwani tunaonekana huenda tukiwa kanisani tunaficha makucha yetu, abadilike.”

2 comments:

mchumi said...

Biashara matangazo

mchumi said...

Biashara matangazo