Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Lu Youqing alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na China
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Imani Njalikai (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Mhe. Lu Youqing ambao hawapo pichani.
Maafisa walioambatana na Balozi Lu wakinukuu mazungumzo akiwemo Kaimu Mkuu wa masuala ya Siasa katika Ubalozi huo, Bw. Li Xhuhang (kulia).
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya (kulia) na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba nao wakisikiliza mazungumzo hayo.
Mazungumzo yakiendelea
WaziriMembe akiagana na Balozi Lu Youqing mara baada ya mazungumzo yao.
Picha na Reginald Philip.
No comments:
Post a Comment