HAMIDA HASSAN
Jamaa ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja, amejikuta akionja joto ya jiwe baada ya kudaiwa kukutwa akiiba kwenye shamba la mahindi hivyo kulazimishwa kula mahindi mabichi.Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye Kata ya Miembeni, Bukoba mkoani Kagera na kuibua gumzo kubwa.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, baada ya kumnasa kijana huyo akiiba mahindi aliyoyajaza kwenye gunia, wamiliki wa shamba hilo walimuamuru kukaa chini na kuyala yakiwa mabichi hadi yaishe, kitendo ambacho jamaa huyo alikubaliana nacho.
lielezwa kwamba, katika hali ya kushangaza, kijana huyo hakukataa wala kuonesha kutetereka kwani alianza kuyala hadi alipoamriwa kuacha na kuambiwa aondoke.Katika habari hiyo iliyoripotiwa na Mtandao wa Harakati, kijana huyo alionekana kuwa na matatizo ya kutosikia vizuri wala kuongea kwa maana ya kuwa ni ‘bubu’.
Hata hivyo, kijana huyo hakujulikana alitokea wapi kwani mbali na madai ya wizi na ububu pia hakuonekana mwenye ufahamu mzuri kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa. GPL


3 comments:
Huu ni uvunjaji wa sheria. Kaiba ndio. Ushahidi upo. Mpelekeni kituo cha polisi. Ale mahindi mabichi kwani yeye nyani? This is inhumane treatment, the suspect has a right to sue waliomlazimisha kula mahindi
Hivi kwa nini watu wanachukua hatua mikononi mwao+hao wanaofanyia watu hivyo wao wana usafi wa kiasi gani? serikali iko wapi?
Kweli kabisa Mdao umesema ukweli mtupu ! Bahati mbaya sio kwa Bongo . Huyo jamaa anabahati kwani wenzake wanavalishwa taili . Nakupigwa kibiriti tu ! Bongo ya sasa mwizi akikamatwa mwenyewe anakimbilia polisi , biashara ya kuwapelekea polisi mhalifu ilishaisha kitaambo! Lakini hii yote imetokananana sisi wenyewe binadamu tulio wengi IMANI zetu zimekua ndogo sana!
Post a Comment