ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 22, 2015

BALOZI WA ZAMANI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA AFANYA MAZUNGUMUZO NA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI WASHINGTON, DC

 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akibadilishana mawili matatu na aliyekua Balozi wa Marekani nchini Tanzania Balozi Mark Green mara tu alipowasili kwenye ofisi za jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani lililopo barabara ya 22 Washington, DC. Balozi Mark Green alikua Balozi wa Marekani nchini Tanzania kuanzia mwaka 2007 mpaka 2009 na mwaka 2014 aliteuliwa kuwa Rais wa International Republican Institute na pia ni mmoja ya wakurugenzi wa bodi yaMillennium Chalenge Corporation (MCC) aliyochaguliwa na Rais Baraka Obama mwaka 2010 na kuchakuliwa tena mwaka 2014
 Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula, Mama Sitti Mwinyi na Bwn. Abdallah Makame Abdallah msaidizi wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakifuatilia mazungumuzo ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Balozi Mark Green 
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akifanya mazungumzo na aliyekua Balozi wa Marekani nchini Tanzania Balozi Mark Green.
 Mazungumzo yakiendelea.
 Kutoka kushoto ni Gretchen Birkle ambaye ni mkurugenzi wa maswala ya Afrika, Balozi Mark Green na Rais mstaafu awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi.

No comments: