ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 22, 2015

Waziri Membe azungumza na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN eneo la Maziwa Makuu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Said Djinnit walipokutana kwa mazungumzo tarehe 22 Aprili, 2015. Katika mazungumzo yao waligusia masuala ya usalama katika Ukanda huo hususan hali ilivyo nchini DRC. 
Waziri Membe akimweleza jambo Bw. Said Djinnit (katikati) huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilshi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez akisikiliza kwa makini. 
Waziri Membe (kulia) akiagana na Bw. Said Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao 

Picha na Reginald Philip

No comments: