ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 22, 2015

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AKABIDHI JEZI KWA MANAHODHA WA BARA NA VISIWANI WASHINGTON, DC


 Balozi wa Tanzania nchini Marekami Mhe. Liberata Mulamula (wapili toka kushoto) akimtambulisha Rais wa Jumuiya ya Watanzania  DMV Bwn. Idd Sandaly na baadae kusalimiana na Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi wakati alipokua akiwasili kwenye jengo la Ubalozi wa Tanzania siku ya Jumatano April 22, 2015 kwa ajili ya kukabidhi jezi kwa manahodha wa timu ya Tanzania Bara na Visiwani kwa ajili ya mtanange utakaochezwa siku ya Jumamosi April 25, 2015 katika maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wengine katika picha ni Mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka na mwakmbata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Colonel Adolph Mutta.
Mhe. Liberata Mulamula akimkaribisha chumba cha mikutano cha Nyerere Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kusalimia baadhi ya Watanzania waliongozana na manahodha wa timu na Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi na baadae kukabidhi jezi kwa manahodha hao.

Kutoka kushoto ni Mama Sitti Mwinyi, Rais mstaafu awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula

Balozi Liberata Mulamula akitoa utambuilisho kwa wafanyakazi wa Ubalozi na kutoa historia ya jengo la Ubalozi kwa Mhe. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kabla hajamkaribisha kuwasalimia baadhi ya Watanzania waliokua wamefuatana na manahodha wa timu ya Bara na Visiwani na wafanyakazi na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Pia Balozi Liberata Mulamula alitoa shukurani za dhati kwa Peoples Bank of Zanzibar (PBZ) kwa udhamini wao wa shughuli nzima ya sherehe ya Muungano ukiwemo udhamini wa mechi ya mpira wa miguu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa salamu toka nyumbani.

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya Bara Bwn. Raymond Abraham wengine kushoto ni Fadhili Londa na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly.

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya Visiwani Seif Ameir

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly akitoa shukurani zake kwa Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwemo Maofisa na wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuwapa nafasi na kutumia muda wao na hatimae kufanikisha makabidhiano ya jezi zitakazo chezewa siku ya Jumamosi April 25, 2015 Walker Mill. Pia Idd Sandaly aliwashukuru PBZ kwa kufanikisha sherehe ya Muungano.

Manahodha wa timu ya Bara na Visiwani na baadhi ya wachezaji wa timu hizo wakipata picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.

Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi





No comments: