Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi akichangia wakati wa mkutano huo, ambapo pamoja na mambo mengine alielezea uzoefu wa Tanzania ambao ni ule wa viongozi wa madhehebu ya kiislam na kikikristo wa kukaa pamoja na kujadiliana changamoto mbalimbali pamoja na kuzitafutia ufumbuzi kupitia umoja wao. vile vile akasema kwamba jitihada za kukabiliana na changamoto zitokanazo na itikadi kali za kidini na ukereketwa wa kupindukia zinatakiwa zifanywa na kumilikiwa na nchi husika pasipo kuingiliwa na mataifa kutoka nje. Aidha amesisitiza haja na umuhimu wa kuangalia na kutafutia ufumbuzi matatizo ya kiuchumi na kijamii ambayo yanawafanya vijana ambao wanakosa fursa ya kuendesha maisha yao kujiingiza katika vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kidini au ya utaifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini mara baada ya viongozi hao wa dini kuzungumza katika mkutano wa ngazi ya juu uliojadili pamoja na mambo mengi kuongezeka kwa vurugu zitokanazo na itikadi kali za kidini na ukereketwa wa kupindukia na nini kifanyike kukabiliana na changamoto hiyo. katika picha hii yupo pia Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutessa ambaye ndiye aliyandaa mkutano huo
No comments:
Post a Comment