ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 13, 2015

DKT. SHEIN AONGOZA VIGOGO KUCHANGIA MAENDELEO YA MKOA WA MJINI MAGHARIB, UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Shilingi za Kitanzania Millioni thalathini kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowasa wakati hafla ya chakula cha hisani kuchangia mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini Kichama katika ukumbi wa Salama Bwawani usiku wa kuamkia Aprili 13, 2015
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Shilingi za Kitanzania laki tano kutoka kwa Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stephen Wasira wakati hafla ya chakula cha hisani kuchangia mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini Kichama katika ukumbi wa Salama Bwawani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar (kulia) alipokuwa akitoa nasaha zake wakati wa Chakula cha hisani cha kuchangia Mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini uliofanyika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja na kuwajumuisha wafanyabiashara mbali mbali na Viongozi wa CCM wa Mkoa huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Shilingi za Kitanzania laki tano kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza wakati hafla ya chakula cha hisani kuchangia mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini Kichama katika ukumbi wa Salama Bwawani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimakabidhi cheti maalum Mama Mwnamwema Shei kwa Mchango wake alioutoa wakati wa Hafla ya chakula cha hisani cha kuchangia mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini Kichama katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja (katikati) Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Borafya Silima Juma(katikati) 
Baadhi ya waalikwa na wafanyabishara wakichukua Chakula wakati wa hafla ya Chakula cha hisani cha kuchangia Mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini Kichama katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ALi Iddi akiwaongoza Viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi katika kuchukua chakula wakati wa hafla maalum ya chakula cha hisani cha kuchangia mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini kichama katika ukumbi wa salama Bwawani Mjini Unguja

5 comments:

Anonymous said...

Where do these leaders get all zat money? Can TUKURU tell us please?

Anonymous said...

Milioni thelathini!!!! Ama kweli!! Mh!'

Imelda Kagyabukama said...

Shule zimefungwa wanafunzi hawana chakula.
Shs 30.000 000/= shule ngapi zingebaki masomoni.
Jamani hii ni kufuru.
Aibu kwa nchi.

Anonymous said...

Mimi sielewi, in the first instance, how did they get all that money to dish around? Na hii is not the first time, they have been doing is around the country.

Anonymous said...

Ni vema kabla hamjawapigia kura mkawauliza hayo maswali..