Advertisements

Friday, April 3, 2015

IBADA YA MISA NA KUAGA MWILI WA MZEE EDDIS MGAWE SILVER SPRING, MARYLAND

Jeneza lililobeba mwili wa mpendwa Mzee Eddis Mgawe likiwa mbele ya Kanisa la Bethel World Outreach Church Lililopo Silver Spring, Maryland ilikofanyika Ibada ya misa ya kumuaga Mzee Eddis Mgawe siku ya Alhamis April 2, 2015 na Watanzania DMV na wengine kutoka majimbo mengine kujumuika pamoja na familia wakiwemo wafanyakazi wa Voice Of America (VOA) wakiongozwa na mkuu wa kitengo hicho cha idhaa ya kiswahili Dr. Hamza Mwamoyo. Mtoto wa marehemu, Mary Mgawe ni mfanyakazi wa idhaa ya Kiswahili ya VOA na wafanyakazi wenzake walimchangia fedha za rambirambi.
Familia ikiaga mwili wa mpendwa wao na wapili toka kushoto ni mke wa marehemu mama. Immaculate Mgawe.
Familia ikiwa na hudhuni kubwa huku watoto wa marehemu wakimfariji mama yao.
Mtunza mahesabu kamati ya msiba Bi. Seche Malecela akiongea kwenye ibada ya misa na kuaga mwili wa mzee Eddis Mgawe iliyofyanika siku ya Alhamisi April 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Mchungaji Dr. Nicku akifanya akifungua Ibada ya misa na kumuaga mzee Eddis Mgawe kwa maombi.
Mchungaji Igogo akiongoza Ibada.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akiongea machache na kusisitiza upendo na mshikamano kwenye Jumuiya zetu.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Juu na chini Watanzania wakiaga mwili wa mpendwa mzee Eddis Mgawe.
Picha juu na chini Watanzania wakijumuika na familia kwenye misa ya kumuaga mpendwa baba yao huku wakitoa pole kwa wafiwa.
Familia ikiaga mwili wa mpendwa wao mara nyingine baa da ya misa kwisha
Jeneza lenye mwili wa mpendwa mzee Eddis Mgawe likiingizwa kwenye gari kuelekea uwanja wa ndege
Picha chini n za ukumbi wa chskula

No comments: