ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 28, 2015

KUFUATIA KIFO CHA MMAREKANI MWEUSI FREDDIE GRAY, WAANDAMANI WAPAMBANA NA POLISI MJINI BALTMORE

Gloria Darden, mama mzazi wa kijana Freddie Gray aliyekufa akiwa mikononi mwa polisi akiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa mtoto wake wakati wa maziko yake.
Mazishi ya kijana Freddie Gray aliyekufa akiwa mikononi mwa polisi yakifanyika
Vurugu kubwa ziliibuka jana katika mji wa Baltmore kati ya polisi na waandamanaji waliokasirishwa na kifo cha kijana Mmarekani mweusi, Freddie Gray aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi. 

Hali ya hatari na kutotembea hovyo imetangazwa katika mji huo kufuatia vurugu hizo.
Katika vurugu hizo, ulitokea uharibifu mkubwa wa maduka, magari na jeshi la polisi nalo limetoa taarifa likisema baadhi ya maofisa wake wamejeruhiwa kufuatia vurugu hizo.
Hali ya hatari na kutotembea hovyo imetangazwa katika mji huo kufuatia vurugu hizo.
Gari la polisi likiteketea kwa moto kufuatia vurugu katika ya waandamanaji na polisi katika mji wa Baltmore, Maryland nchini Marekani hapo jana.
Polisi wakiwa wamejipanga tayari kupambana na waandamanaji katika mji wa Baltimore, baada ya maziko ya kijana Freddie Gray ambaye ni Mmarekani mweusi aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi.
Kifo cha Freddie Gray ambaye ni kijana mweusi mmarekani mwenya asili ya kiafrika kimesababisha maswali mengi kuhusu matumizi ya nguvu za ziada ya polisi dhidi ya raia wa marekani wenye asili ya kiafrika.
Hata hiyo Msemaji wa polisi wa Baltimore Captain Eric Kowalczyk amesema vurugu hizo pia zimesababisha maafisa wake kujeruhiwa na wengine wapo katika hali mbaya.
Askari polisi wakimsaidia mwenzao baada ya kujeruhiwa na waandamanaji

6 comments:

Jay said...

Muda umefika kwenu wabongo mliopo huko majuu kurudi nyumbani, hakuna chochote huko cha maana. Wamarekani weusi wanajihaibisha wenyewe na si watu wanaopenda kufanya kazi. Utumwa umekwisha ila wao mpaka leo hii bado wanaishi kiutumwa na hawataki kujituma ila kusubiri vya bwerere tu toka serikalini. Jiulizeni, kwanini wanaishi ghetto mpaka leo hii?

Anonymous said...

sasa wewe bwege 12:56 hiyo statement yako inausiana nini na wabongo kurudi nyumbani?

Anonymous said...

Sasa inahusiana nini na wabongo kurud tanzania lol yetu yanaenda

Anonymous said...

@&$???!

Anonymous said...

Tukirudi bongo tutafanya nini lamaana? Kuuza chupi?

Anonymous said...

wewe unayesema wabongo warudi TZ kiazi kweli. Kwani kwenye picha hizo unaona au umesoma wapi wa TZ wananyanyaswa? Usikurupuke ndugu yangu, hii sio South Africa.