Wananchi wa Burundi wameandamana na kusababisha fujo kubwa na polisi wa nchi hiyo. Hii ni baada ya Rais anaeondoka madarakani Bwana Pierre Nkurunzinza kukataa kuachia madaraka na kuamua kugombea awamu nyingine ya tatu kinyume na katiba ya Burundi.
Polisi wa kuzuia fujo wa Burundi wakitumia nguvu dhidi ya wananchi.Rais Nkurunzinza na wafuasi wake wamesema muhula wa kwanza wa rais huyo hauhesabiki kwa maana aliteuliwa na bunge la nchi hiyo. Hivyo anaweza gombea muhula mwingine.
Rais mstaafu bwana Pierre Buyoya ameonya kwamba hatua ya rais Nkurunzinza inaweza tumbukiza nchi ya Burundi kwenye vita nyingine.
No comments:
Post a Comment