ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 26, 2015

Mahojiano ya Kamanda Ras Makunja na Zenj FM, asema Wanamuziki wa Bongo watoe kazi zao nje ya nchi

Wanamuziki wa Bongo Msiogope Kutoa kazi Zenu nje ya nchi ! Mnakubalika-
Asema Ras Makunja.

Katika mahojiano ya Ras Makunja kiongozi wa Ngoma Africa band iliyopo kule
nchini ujerumani na Zenj FM katika kipindi maalumu cha muziki wa dansi kinaongozwa na mtangazaji mahiri bwana Mustapha Mussa siku ya jumamosi 25 April 2015.
Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja akihojiwa kwa njia ya simu alikuwa akijibu maswali ambayo majibu yake yamesikika kama ni pumzi mpya ya uhai wa muziki wa dansi Tanzania na miziki mingine kama vile taarabu na muziki wa kizazi kipya,Kamanda Ras Makunja ametoa wito kwa wasanii wa Tanzania wasisite wala kuogopa kutoa kazi zao nje ya mipaka ya nchi kwani Tanzania inajulikana kuwa ina muziki mzuri na unao kubalika kimataifa "Wanamuziki Msiogope tuone kazi zenu nje mnatisha na kukubalika" alitoa wito
Mkuu huyo wa Ngoma Africa Band aka FFU kamanda Ras Makunja,ambaye pia
aliwasifu sana wanamuziki wa wakongwe wazamani kuwa ndio kioo cha wanamuziki wengine.
Alipoulizwa umri wa bendi ya Ngoma Africa kamanda Ras Makunja amesema bendi inatimiza miaka 22 na imekuwa sawa na muzimu wa muziki unao mtisha hata yeye mwenyewe unamtisha ! pia alichambua changamoto zinazoukabili muziki wa dansi nyumbani Tanzania,ni pamoja na baadhi ya vituo vya redio kutopiga mara kwa mara nyimbo za bendi za dansi,pia aliwaomba wanamuziki na bendi za muziki wa dansi kufupisha nyimbo zisiwe ndefu mno,na aliwaomba kuacha tabia ya kulalamikia kitu au hali fulani baadala yake kujitaidi kuutangaza
muziki wa dansi katika kila hali na kuvifuata vyombo vya habari sio kusubiri.
fuatilia mahojiano hayo katika Redio Zenj FM ya Zanzibar.
pia unaweza kuwasikiliza FFU at www.ngoma-africa.com

No comments: