
Kiongozi wa Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa jana. Picha na Said Ng’amilo
Dar es Salaam. Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kila mwanachama anapaswa kuwaunga mkono wagombea watakaopitishwa na chama hicho katika nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwani kinyume chake ni kukisaliti na adhabu yake ni kufukuzwa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira alisema mwishoni mwa juma kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, chama hicho kinahitaji nguvu za pamoja.
“Sisi bado hatujajiunga na Ukawa, hivyo wanachama wetu wanapaswa kulitambua hilo na kuepuka kushiriki kwenye ushawishi wa kufanya kampeni za wagombea wa vyama vingine. Hata kwenye katiba yetu tunasema sasa tunalenga zaidi katika kujiimarisha ili kutoa ushindani mzuri wa kisiasa katika uchaguzi huu,” alisema.
Katiba ya ACT, imeeleza wazi kuwa pamoja na sababu nyingine na kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati chama kimeweka mgombea wake kwa mujibu wa sheria za nchi, atakuwa amepoteza uanachama wake.
ACT- Wazalendo tayari imetoa ilani yake ya uchaguzi ikionyesha kwamba iwapo itaingia madarakani, itawajibika kwa wananchi kwa kuweka kipaumbele katika maeneo manne ambayo ni hifadhi ya jamii, uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, afya na elimu.
Kauli hiyo ya ACT linakuja huku kambi ya vyama kadhaa vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ikiwa kwenye mchakato wa kuunganisha nguvu ili kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo katika baadhi ya maeneo.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amewahi kunukuliwa akisema kuwa umoja huo unaoundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD umehamishia nguvu zake kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Mbatia alisema tayari umoja huo umeunda kamati maalumu kutafuta namna ya kumsimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema tayari kamati zimeundwa na zinaendelea na kazi ya kuratibu mpango huo mahsusi, unaolenga kuiondoa CCM madarakani.
“Lengo letu ni kuhakikisha Ukawa ina nguvu ya kushika dola katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na katika mpango huo, vyama vitaachiana majimbo na viti vya udiwani kulingana na nguvu ya chama katika sehemu husika,” alisema.
Mkakati huo uliopangwa na Ukawa, unaelezwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa ni kombora kwa CCM, kwani endapo utafanikiwa, utakiweka chama hicho tawala katika wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu uliopangawa kufanyika Oktoba mwaka huu.
MWANANCHI
5 comments:
We said, and we will continue to say that ZITTO ni kibaraka. Kama kweli anataka serikali iliyoko madarakani iondoke kwa demokrasia ya "kura za wananchi" basi anachokifanya ni kujaribu kupunguza kura za "ukawa". tulisema mwanzoni kabisa hata kabla ya yeye (zitto) kuondoka chadema. Ni kibaraka na anapenda sana madaraka Mheshimiwa Zitto! Kama una ubavu wa kisiasa ambao hujakingiwa kifua na "watu" basi ingia kwenye ulingo huu tupambane kwa hoja hapa!
Wana ACT wa Zitto. Haya mawimbi yana kasi lakini upepo utayumba na mawimbi yataishia baharini! Siasa za aina yake! Watizame wenzako waliojiita gwiji na wako wapi sasa. Kazi kwelikweli!
People are just curious to hear whats new ,whats his agenda... but after the rally very few seem to be influenced....People dont get a point from him # i GUESS
mchawi huyu kijana,watu wanalia na hali mbaya iliopo anatoboa mtumbwi karibia kutia nanga akijua kuna wazee na wagonjwa wasio weza kuogelea,mwenye mawasiliano nae amwambie nimesema ni mchawi tu aweza fanya afanyayo huyu kijana na chama chake, akome
Ukisoma between the lines utaona kuwa ACT sio segment ya CCM bali ni chaka la baadhi ya wana CCM.na ACT itaenda kuibomoa CCM big times.hii kutegemeana na mazingira yatakavyokuwa wakati wa lala salama ya kuelekea uchaguzi mkuu inaweza au isiweze kuisaidia ukawa.
Post a Comment