Fatma Kassim akiimba.
MASHABIKI wa taarab nchini jana walipata walichokitaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.Katika onyesho la jana, Kundi la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf lilimwaga burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki kibao waliofurika katika ukumbi huo ambao una kila aina ya ‘mafuraha’ ikiwa ni pamoja na makulaji na vinywaji licha ya hali ya hewa kujenga tishio la mvua kila mara.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)
No comments:
Post a Comment