ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 11, 2015

MKUTANO WA CUF KESHO JUMAPILI JIMBO LA KITOPE

The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinawatangazia na kuwaalika wazanzibari wote kushiriki katika Mkutano wa hadhara wa aina yake, ulioandaliwa na Chama hicho siku ya Jumapili, tarehe12/04/2015.

Mkutano huo utafanyika katika Jimbo la Kitope, kiwanja cha Kitope Kipandoni kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni(8:00-12:00) na kuhutubiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Tukumbuke kwamba Jumapili ya tarehe 12/04/2015 ni siku maalum, katika eneo maalum, kwa ajili ya shughuli maalum.

Tuungane kwa pamoja katika siku hii ya aina yake kuudhihirishia ulimwengu kwamba CUF haitokubali kutolewa katika mstari wa kudai Mamlaka Kamili ya Zanzibar na itahakikisha inashinda uchaguzi wa 2015 na inatangazwa kwa kutumia njia za kidemokrasia.

No comments: