Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akisaini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Bohari ya Dawa (MSD), katika maonyesho ya kuadhimisha siku ya malaria yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alipotembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga na ofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
Maofisa wa MSD wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga, Ofisa wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa MSD, Emmanuel Kais, Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla, Ofisa Habari, Benjamin Massangya na Dereva, Said Tindwa.
Baadhi ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vinaoneshwa.
Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga (kushoto), akimuelekeza jambo kijana aliyetembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick,
ameitaka Bohari ya Dawa MSD kuendeleza
kasi ya huduma zake za kupambana na ugonjwa wa malaria kwakuwa ni moja ya taasisi zilizo mstari wa mbele kupunguza vifo
vitokanavyo na ugonjwa huo.
Akizungumza jana katika banda la MSD ikiwa ni
maadhimisho ya siku ya Malaria duniani Sadick alisema MSD imekuwa ikifanya
jitihada kuhakikisha ugonjwa wa malaria unakoma na vifo vitokanavyo na ugonjwa
huo vinapungua.
Alisema jitihada hizo za MSD zimechangia
matokeo ya kupungua takwimu za vifo vya mama na mtoto mchanga chini ya miaka
mitano vitokanavyo na ugonjwa wa malaria hivyo jitihada zaidi zinahitajika
kuhakikisha malengo ya millennia ya kupunguza vifo hivyo yanafikiwa.
Alisema kutokana na MSD kuhakikisha dawa za
malaria zinapatikana katika kila kituo cha afya, Zahanati na Hospitali ni
wajibu wa wananchi kuhakikisha wanafanya
matumizi sahihi ya dawa hizo ili kutibu ugonjwa huo.
“MSD inasaidia serikali kufikia lengo la
kupunguza ugonjwa wa malaria tumeelezwa jinsi gani MSD inahakikisha dawa za
malaria hazikosekani katika vituo vya kutolea huduma lakini pia imepanua wigo kwa kutoa elimu kwa vitendo jinsi ya
kupambana na ugonjwa huo kwa kuhakikisha
kinga dhidi ya malaria inaanzia kwa wafanyakazi wake na wanapewa
vyandarua vyenye dawa wao na familia zao,”alisema
Sadick aliwataka wananchi kuacha kutumia dawa
hizo katika matumizi yasiyo sahihi ikiwemo dozi moja ya dawa kutumiwa na watu
zaidi ya mmoja kwakuwa kufanya hivyo kunasababisha matibabu ya wagonjwa wa
malaria kutokukamilika na kusababisha vifo.
Alisema pia kumekuwepo na matumizi yasiyo
sahihi katika vyandarua vya msaada
ambapo utumika kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki hivyo mapambano
dhidi ya ugonjwa huo kutokufanikiwa.
“ Jitihada hizi za MSD na wafadhili mbalimbali
katika kuweka nguvu ya kupambana na Malaria ni wajibu wa jamii kuziunga mkono kwakuwa matumizi ya
misaada hiyo ikiwemo Vyandarua ikitumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi
kutokana na kuimarika kwa afya ya wananchi wake,”alisema.
Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo alizindua
mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za
Serikali na wadau mbalimbali kupambana na ugonjwa wa Malaria. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)
No comments:
Post a Comment