Advertisements

Thursday, April 2, 2015

MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA AACHIWA KWA DHAMANA DODOMA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, (mwenye koti la kahawia), akisindikizwa na mawakili na wafanyabiashara wenzake.


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja ameachiwa kwa dhamana leo jijini Dodoma baada ya kushikiliwa kwa siku sita kufuatia kuondolewa dhamana ya awali kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana.

Minja ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma ikiwa ni siku moja baada ya suala lake kuibuliwa bungeni mjini Dodoma kwa baadhi ya wabunge kuitaka serikali kukaa na kuangalia namna ya kuweza kumaliza mgogoro uliopo kwa kupatiwa dhamana kwa mwenyekiti huyo.

Kushikiliwa kwa Minja kumesababisha kuwepo migomo ya wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali nchini waliokuwa wamefunga maduka yai kushinikiza kuachiwa kwa mwenyekiti wao huyo

No comments: