ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 24, 2015

NAIBU WAZIRI WA MAJI MHE. AMOS MAKALLA ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAJI MUFINDI NA SONGEA

Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akisalimiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Mufindi mara baada ya kuwasili.

Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Mufindi na Songea. Akiwa wilayani Mufindi, Mh Makalla amekagua mradi mkubwa wa Maji wa ikilimanzoo na kuelekeza mkandarasi aukamilishe haraka.  Aidha Naibu Waziri huyo wa Maji amekagua na kutoa cheti kwa jumuiya ya watumia maji Mkongotema na Magingo (MAMKO). 
Leo Ijumaa  ataendelea na ziara yake wilaya ya Namtumbo kukagua miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa na serikali.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akifungua bomba la maji lililopo katika moja ya vituo vya mradi wa maji katika kijiji cha Magingo kilichopo tarafa ya Madiba kijiji cha Mkongotema mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Katibu wa CCM Wilaya ya Songea ndugu Rajabu Uhonde.

Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akitembea kwenda kukagua tenki la maji katika kijiji cha Magingo, kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea ndugu Juma Ally.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akimtwisha ndoo ya maji mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Magingo.
Mwanafunzi wa shule ya Magingo akifurahia kupata maji baada ya kutatuliwa tatizo la maji lililo wakabili kwa muda mrefu, pembeni ni Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akihakikisha ndoo ya maji aliyobeba mwanafunzi huyo imekaa sawa sawa kichwani.

No comments: