Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akienelea kuwapungia mkono kwa furaha kuwasalimia wananchi
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na Viongozi wengine wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
4 comments:
Huu Si Muungano
Ni nchi moja kuitawala Nchi Nyengine Kwa Mabavu
Tanganyika kuitawala Zanzibar
UN stop Tanganyika to Colonize Zanzibar
Si mjitoe kama mnaona mnatawaliwa
Wewe utakuwa ni mwaarabu siyo Mtanzania. Unaweza kurudi makwenu uarabuni kama huupendi muungano wetu. UN haikutuunganisha,bali ni sisi watanganyika na wazanzibari wenyewe ndiyo tuliungana. Nadhani ulikuwa bado hujazaliwa kule uarabuni.
Wewe hapo juu ndiyo umekosea it clearly shows zanzibar ndiyo mnafaidika na muungano fake huu. Its time tanganyika iwe huru na zanzibar ibaki peke yake maana mpaka leo mnaserikali yenu na kujiita wa zenji. Tuache kudanganyana ....mtoto akililia wembe...mpe so wazenjj hawataki muungano so tuwabwage maana hamna lolote tunalofaidika zaidi yakulipia kodi and ccm ndiyo chanzo.
So kabla wazenj hamja oiga kelele za kijinga waambiyeni viongozi wenu mnachotaka na wa tanganyika pia tufanye hivyo hivyo na kupiga kura ya kubaki na muungano au kuvunja kwani hata ndoa zinavunjika. Tusibaki kupigizana kelele za kijinga wakati wakubwa wanaenjoy pesa
Post a Comment