Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania unapenda kutoa shukurani kwa watanzania wote kwa kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe za muungano, Mpira, BBQ na Muungano Night.
Pia tunapenda kumshukuru Rais Mstaafu Muheshimiwa Ali Hassan Mwinyi kwa kujumuika na sisi katika sherehe hizo.
Uongozi unapenda kumshukuru balozi wetu Liberata Mulamula Kwa kushirikiana na kujumuika na sisi kwenye sherehe hizi.
Shukurani maalumu ziwafikie People Bank of Zanzibar(PBZ) kwa kudhamini Mpambano wa mechi ya Soccer kwa mwaka wa pili mfululizo. Na tunawaomba wana DMV tushirikiane na PBZ pia.
Vilevile Uongozi unatoa shukurani kwa kamati, Vijimambo blog na wafanyakazi wa ubalozi katika kushiriki na kusaidia kwenye kukamilisha shughuli hizi za sherehe za Muungano.
Kwa hakika uongozi unapenda kuipongeza Timu ya Zanzibar Heroes kwa Kutwaa kombe la muungano.
Wenu
Iddi Sandaly
President
ATC- DMV
No comments:
Post a Comment